Vyombo ya habari nchini Kenya havina uzalendo? | Matukio ya Afrika | DW | 30.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Vyombo ya habari nchini Kenya havina uzalendo?

Nchini Kenya waandishi habari wanadaiwa kutokuwa na uzalendo kwa namna wanavyoripoti juu ya masuala ya ugaidi yanayoendelea nchini humo.

Waandishi wa habari nchini Kenya wakiwa kazini

Waandishi wa habari nchini Kenya wakiwa kazini

Joseph Kaguthi mwenyekiti wa kitengo cha kitaifa kinajumuisha jamii katika maswala ya kutoa taarifa za kiusalama kwa polisi amesema waandishi habari hawapaswi kuungana na magaidi kwa namna wanavyoandika habari zao. Kaguthi amesema kila Mkenya anafahamu kuwa wanajeshi walioko Somalia wanapigana na magaidi kwa hivyo vita hivyo vinapaswa kuungwa mkono na vyombo vya habari. Amina Abubakar alizungumza na Joseph Kaguthi na kwanza alitaka kujua kipi anachomaanisha anaposema vyombo vya habari nchini Kenya havina uzalendo kwa nchi yake.

Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi:Amina Abubakar

Mhariri:Yusuf Saumu

Sauti na Vidio Kuhusu Mada