Vyama vya madaktari Ghana vyaonya mfumo wa afya kulemewa | Matukio ya Afrika | DW | 10.07.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Vyama vya madaktari Ghana vyaonya mfumo wa afya kulemewa

Huenda mfumo wa afya utalemewa iwapo serikali itakosa kuchukua hatua za haraka. Vyama vya madaktari nchini Ghana vimeonya.

Vyama vya madaktari na wahudumu wa afya nchini Ghana vimeonya kuwa huenda mfumo wa afya ukaelemewa iwapo serikali itakosa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha usalama wa wahudumu wa afya.

Kupitia taarifa ya pamoja, vyama hivyo vimesema kuwa wahudumu wa afya 779 wameambukizwa virusi vya Corona kufikia mwisho wa mwezi Juni.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa hali hiyo imelemeza utoaji wa huduma za matibabu hasa wakati huu ambapo idadi ya wagonjwa wa Covid-19 inazidi kuongezeka.

Onyo hilo wamelitoa baada ya kufanya mkutano wa dharura mnano Julai mosi.

Nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika imerekodi maambukizi 23,000 ya Covid-19 na vifo 129 vilivyotokana na ugonjwa huo.