1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vurugu zatawala uchaguzi wa Cameroon

10 Februari 2020

Cameroon ilipiga kura Jumapili iliyopita katika uchaguzi uliogubikwa na matukio ya wapinzani kuususia katika baadhi ya maeneo na kuzuka kwa vurugu zilizopelekea mamia kwa maelfu ya watu kukimbia makaazi yao

https://p.dw.com/p/3XZB8
Kamerun Präsidentschaftswahlen 2018
Picha: Reuters/Z. Bensemra

Uchaguzi huo wa wabunge na serikali za mitaa katika nchi hiyo ya Afrika ya kati umefanyika kwa mara ya kwanza katika kipindi cha mika saba baada ya kuahirishwa mara mbili.

Lakini kutoshiriki kwa wapinzani katika uchaguzi huo kunamanisha ya kwamba hakutaathiri utawala wa Rais Paul Biya mwenye umri wa miaak 86, mmoja wa viongozi wa zamani duniani waliokaa madarakani kwa muda mrefu ambaye ameshikilia madaraka kwa miaka 37.

Wakati ambapo kura zikipigwa, idadi kubwa ya askari polisi na wanajeshi walitapakaa katika mitaa ya Buea, makao makuu ya mkoa wa Kusini Magharibi ambao ni miongoni mwa mikoa miwili inayoshuhudia matukio ya umwagaji damu kutokana na harakati za kujitenga.

Vituo vya kupigia kura ndani ya jiji vilikuwa kimya na hakukuwepo na vurugu zozote zolizoripotiwa na kulikuwa na wapiga kura wachache. Kura nyingi za asubuhi zilishuhudiwa zikipigwa na maafisa wa usalama waliopelekwa kwa ajili ya kutuliza amani.

"Shughuli za upigaji kura zimekamilika katika nchi nzima katika vituo 26,336 kwa utulivu na kufuata sheria na nidhamu."Alisema Erik Essousse, mkurugenzi mkuu wa tume ya uchaguzi alipowaambia wandishi wa habari.

Chama kikuu cha upinzani cha Movement for the Rebirth of Cameroon (MRC) kilikataa kuweka mgombea wao.

Chama kingine kikuu cha upinzani cha Social Democratic Front (SDF) ambacho kwa sasa kina viti 18 kilishiriki uchaguzi wa huo wa jumapili