Vurugu zaendelea Zanzibar | Matukio ya Afrika | DW | 19.10.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Vurugu zaendelea Zanzibar

Vurugu visiwani Zanzibar ambazo zinazojitokeza huko sasa zimeanza kuonekana kuleta mvutano katika baraza la wawakilishi.

Wakuu wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar

Wakuu wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar

Tangu jana na leo asubuhi (19.10.2012) wajumbe wa baraza hilo kutoka upande wa chama cha CCM walisusia kuingia vikaoni wakilalamika kuhusu fujo hizo na kulituhumu kundi la Jumuiya ya Uamsho kuwa linahusika.

Wajumbe hao wanadai kundi hilo ni wafuasi wa chama cha CUF ambacho ni mshirika katika serikali ya muungano visiwani humo.Pamoja na hayo hali ya usalama bado si Shwari huku wasiwasi ukiendelea umetanda hasa baada ya tangazo la hapo jana la kundi hilo kwamba linajiandaa hii leo kumtafuta kiongozi wa jumuiya ya taasisi za kiislamu Sheikh Farid Ahmed aliyetoweka kwa siku kadhaa sasa. Polisi inadai haifahamu wapi alipo au nani anahusika na kisa hicho. Salma Saidi kutoka Zanzibar anaifuatilia hali ilivyo na kwa sasa ametutumia taarifa ifuatayo.

(Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Mohammed AbdulRahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada