Vladmir Klitschko ahifadhi taji lake la dunia | Michezo | DW | 27.04.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Vladmir Klitschko ahifadhi taji lake la dunia

Bingwa wa ndondi wa Ukraine Vladmir Klitschko ametetea kwa urahisi mataji yake ya dunia ya uzito wa juu baada ya kumwangusha sakafuni mpinzani wake Muaustralia Alex Leapai katika raundi ya tano ya pigano

Pigano hilo la jana usiku lilifanyika katika mji wa magharibi ya Ujerumani Oberhausen. Miongoni mwa mashabiki waliokuwepo kumshangilia Klitschko ni kaka yale ambaye ni mwanasiasa maarufu nchini Ukraine Vitali Klitschko. Baada ya kutetea mataji yake ya WBO; WBA; IBO; na IBF, Klitshcko mwenye umri wa miaka 38, alisema ushindi huo ni wa watu wa Ukraine wanaokabiliwa na mzozo unaeondelea wa kisiasa.

Klitschko ambaye hakuwahi kushindwa kwa miaka 10, alisema pigano la jana halikuwa rahisi, kwa sababu kichwa chake kilikuwa na raia wenzake wa Ukraine. “kinachoendelea nchini mwangu ni suala la wasiwasi kwa dunia nzima“. Alisema Klitschko aliyemwangushia mpinzani wake makonde 147 ikilinganishwa na kumi pekee yaliyorushwa na Leapai.

Klitschko alishinda pigano la 53 kwa njia ya knock out maishani mwake katika ushindi wake wa 62 kati ya mapigano 65 ya kazi yake na refarii hatimaye aliingilia kati baada ya dakika mbili, sekunde tano za raundi ya tano. Lakini bingwa huyo alimsifu mpinzani wake akisema aliendelea kupigana kwa ujasiri. Leapai amesema ni wakati wa yeye kujifunza na sasa anarudi katika chumba cha mazoezi kwa sababu huu sio mwisho wake.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohammed Dahman