1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Amerika Kusini yafanya mkutano wa kuikaribisha Brazil

Bruce Amani
24 Januari 2023

Marais 15 wa Amerika Kusini wanakutana leo mjini Buenos Aires katika mkutano wa kikanda wa kuikaribisha tena Brazil.

https://p.dw.com/p/4Mdda
Argentinien l Brasilianischer Präsident Lula da Silva trifft Präsident Alberto Fernández
Picha: Esteban Collazo/Argentinian Presidency/AFP

RaisLula Inacio Lula da Silva akilenga kujenga upya mahusiano baada ya mtangulizi wake wa siasa kali za mrengo wa kulia Jair Bolsonaro kujiondoa katika kundi hilo.

Lula mwenye umri wa miaka 77, ambaye yuko Argentina kwa ziara yake ya kwanza ya kimataifa ya muhula wake wa tatu, anashiriki katika mkutano wa kilele wa saba wa Jumuiya ya Mataifa ya Amerika Kusini na Caribbean - CELAC, unaoyaleta pamoja mataifa 33 kutoka kanda hiyo.

Lula ni mmoja wa waasisi wa CELAC ambalo ni jukwaa la mashauriano na ushirikiano.