1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Umaro Sissoco Embaló und Offiziere der Armee
Picha: Präsidentschaft der Republik Guinea-Bissau

Viongozi wa Afrika Magharibi wakutana baada ya mapinduzi

Iddi Ssessanga
3 Februari 2022

Viongozi wakuu wa mataifa ya Afrika Magharibi leo wanafanya mkutano muhimu wa kilele, wakati ambapo kanda hiyo inayopambana na umaskini ikikumbwa na wimbi la mapinduzi ya kijeshi. 

https://p.dw.com/p/46Ryx

Mazungumzo hayo ya dharura yanayofanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra, yameitishwa baada ya Burkina Faso hapo Januari 24, kuwa taifa la tatu katika kanda hiyo ambapo jeshi limetwaa madaraka kupitia mapinduzi.

Burkina Faso imefuata katika nyayo za Mali, ambako mapinduzi ya Septemba 2020 yalifuatiwa na ya pili Mei 2021, na Guinea, ambako rais aliechaguliwa Alpha Conde alipinduliwa Septemba mwaka jana.

soma zaidi: Rais wa Guinea-Bissau anusurika jaribio la mapinduzi

Shambulio la bunduki siku ya Jumanne dhidi ya rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo, liliongeza hofu kwamba juhudi za miaka kadhaa za kuleta utulivu na demokrasia katika kanda ya Afrika Magharibi zilikuwa zinaelekea kushindwa.

Mkutano huo wa siku moja uliotazamiwa kuanza majira ya saa saba kwa saa za Afrika Mashariki, utatathmini matokeo ya jumbe mbili zilizotumwa Burkina Faso baada ya mapinduzi.