Vimini marufuku kwa wafanyakazi wa umma Uganda
5 Julai 2017Matangazo
Hereni na bangili kubwa nazo zimepigwa marufuku kwa watumishi wakiwa kazini. Watumishi wa umma aidha waliagizwa kutovalia ndala ila tu ikiwa wanafuata ushauri wa daktari. Watu mbalimbali nchini Uganda wamepokea agizo la mavazi ya heshima kwa watumishi wa serikali kwa maoni tofauti tofauti. Mjadala ambao umeibuka ni kama mavazi yana mahusiano yoyote na utendaji kazi wa mtu kazini na kama agizo hilo linalenga kuwanyima wanawake haki zao kujirembesha vile wapendavyo.