Vikosi vya Rwanda vyaelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati | Matukio ya Afrika | DW | 19.01.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Vikosi vya Rwanda vyaelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kwa mara ya kwanza sehemu ya kwanza ya kikosi cha jeshi la Rwanda kimeondoka mjini Kigali kuelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya kati kwa ajili ya ulinzi wa amani nchini humo.

Wanajeshi wa Ruanda

Wanajeshi wa Ruanda

Jeshi hilo limeelekea Jamhuri ya Afrika ya kati likiwa na zana nzito nzito za kivita kama ishara ya kukabiliana na hali yoyote ya vita. Kikosi hicho kimesafiri kwa msaada wa helikopta ya kivita ya jeshi la Marekani.

Mwandishi wetu wa Kigali Sylvanus Karemera amefanya mahojiano na Msemaji wa jeshi la Rwanda Brigedia Jenerali Joseph Nzabamwita ambaye anaanza kwa kuthibitisha kuondoka kwa kikosi hicho na jukumu lake nchini Jamhuri ya Afrika ya kati. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Sylvanus Karemera

Mhariri: Saumu Yusuf

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com