1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vigogo wa Bundesliga kuwapa wapinzani fedha

27 Machi 2020

Vilabu vinne vikubwa vya kandanda la Ujerumani vimeahidi mchango wa euro milioni 20 kuwasaidia wapinzani wao wa ligi kuu ya kandanda - Bundesliga wanaokabiliwa na matatizo ya kifedha katika mgogoro wa virusi vya corona

https://p.dw.com/p/3a6iz
Champions League Fans in London
Picha: picture-alliance/dpa

Vilabu vinne vikubwa kabisa katika kandanda la Ujerumani vimeahidi mchango wa euro milioni 20 kuwasaidia wapinzani wao wa ligi kuu ya kandanda - Bundesliga wanaokabiliwa na matatizo ya kifedha katika mgogoro wa virusi vya corona.

Kitengo kinachosimamia ligi ya Ujerumani - DFL kimesema Bayern Munich, Borussia Dortmund, Bayer Leverkusen na RB Leipzig  -- ambazo zilifuzu katika Champions League msimu huu -- zimejitolea kutoa fedha hizo kwa vilabu vilivyokumbwa na mgogoro. Rais wa DFL Christian Seifert amesema uamuzi huo unadhihirisha ukweli kwamba mshikamano sio neno lisilo na maana yoyote katika Bundesliga.

Vilabu hivyo vinne havitachukua euro milioni 12.5 za sehemu yao malipo yaliyobaki ya mapato ya haki za matangazo ya televisheni kwa msimu ujao, na kuongeza euro milioni 7.5 zaidi kutoka kwenye hifadhi zao.