1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VfL Bochum na Greuther Fuerth zapanda daraja

24 Mei 2021

Timu ya VfL Bochum na Greuther Fuerth zimepanda daraja na sasa zitacheza katika ligi kuu ya Ujerumani - Bundesliga msimu ujao. Holstein Kiel lazima itahitaji kujitafutia tiketi kupitia mechi ya mchujo.

https://p.dw.com/p/3tqKX
Fußball 2. Bundesliga | VfL Bochum - SV Sandhausen
Picha: Guido Kirchner/dpa/picture alliance

Bochum ilipata ushindi wa 3 - 1 dhidi ya Sandhausen na kuchukua ubingwa wa ligi ya Bundesliga daraja la pili na kupandishwa kwa mara ya saba katika historia ya klabu hiyo. Walicheza mara ya mwisho mwaka wa 2006 hadi 2010. Fuerth ilitoka nyuma mara mbili na kuwapiga Fortuna Duesseldorf 3 - 2 na kutinga Bundesliga kwa mara ya pili baada ya msimu wa 2012-13. Bochum na Fuerth zinachukua nafasi za Schalke na Werder Bremen zilizoshushwa kutoka Bundesliga. Kiel ilifungwa 3 -2 na Darmstadt na sasa itacheza na FC Cologne wiki ijayo katika mechi mbili za mkondo wa nyumbani na ugenini