VFB Stuttgart | Michezo | DW | 26.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

VFB Stuttgart

VFB stuttgart ndio mabingwa wapya wa Ujerumani .Waliwaambia mahasimu wao msimu uliopita Schalke na Bremen kuwa kutangulia si kufika.

Timu ya VFB Stuttgart wakisherehekea ushindi katika Bundesliga mwaka huu

Timu ya VFB Stuttgart wakisherehekea ushindi katika Bundesliga mwaka huu

Ilikuwa Mei 19 mwaka hjuu ,siku ya mwisho ya Ligi ndipo Stuttgart iliotoka nyuma kuzipiku klabu 2 zilizokuwa usoni mwake:Bremen na Schalke na kutoroka tena na taji la ubingwa wa Bundesliga.

“Sasa mpira umekwisha na VFB Stuttgart ni mabingwa wa Ujerumani.Hapa viroja vikubwa vinapita hivi sasa.Ni visa ambavyo huonekana tu pale timu inaposhinda katika mchezo wa kispoti.”Alisimulia ripota wa ARD uwanjani.

Mamia ya mashabiki katika kitovu cha jiji la Stuttgart wakiishangiria timu yao pamoja na kocha wao Armin Veh:

“Mkiona kinapita nini hapa,mimi sijafikiria kabisa hata kwenye ndoto kingetokea.” Veh alisema.

VFB Stuttgart inajivunia kutawazwa mabingwa wa Ujerumani jumla ya mara 5 .Juni 26,1950,Stuttgart ilicheza finali ya kuania taji la ubingwa wa Ujerumani katika uwanja wa olimpik wa berlin.Maadui zao walikuwa Offenbacher kickers,lakin I walishindwa kufua dafu mbele ya Stuttgart.

Miaka 2 baadae, chini ya kocha Schorsch Wurzer,Stuttgart ilitoroka tena na ubingwa.Mwongo wa mafanikio m akubwa wa 1950 ulinawirishwa kwa ushindi pia wa vikombe vya shirikisho la dimba la Ujerumani mwaka 1954 na tena 1958.

1963,VFB Stuttgart ikafanikiwa kujiunga na Ligi mpya ilioanzishwa mwaka huo-Bundesliga.Katika Bundesliga, Stuttgart ilizama chini kabisa 1975 walipoteremshwa daraja ya pili.wakati huo huo alishika hatamu rais mpya alieiokoa Stuttgart na kuitoa shimoni:ni mwanasiasa Gerhard Mayer-Vorfelder aliekuja kuwa pia rais wa DFB-shirikisho la dimba la Ujerumani.Alisema,

“Sitaki kuambiwa moyo wangu unadunda kwa Stuttgart.Kwani moyo huu sikuonesha tu katika kikao hiki cha wanachamna kwa kuwa nimechaguliwa bali ningeuonesha hata nisingechaguliwa.”

Nini yeye alieijenga upya Stuttgart na kuiweka katika msingi barabara wachezaji halisi wa kulipwa.1977,Stuttgart ikarejea daraja ya kwanza.Mastadi wake wapya kama akina hansi Muller na karlheinz Förster walitamba hadi katika timu ya taifa.

1984,Stuttgart ilitawazwa kwa mara ya tatu mabingwa wa ujerumani.

Chini ya nahodha Guido Buchwald,Stuttgart iliendelea kutamba katika Bundesliga miaka ya 1980 hadi 1990.Nahodha huyu Buchwald chini ya kocha wa sasa wa Fc cologne, Christoph Daume aliiongoza Stuttgart, kutwaa ubingwa mwengine 1991/92.Stuttgart iliizaba Leverkusen mabao 2:1 na kutoroka na taji.

Kutwaa taji la tatu la kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani hapo 1997,Stuttgart ikicheza na mastadi wake 3-mbrazil Giovani Elber,Bobic na Balakov,ililaza Cottbus.

Msimu mpya ukianza mwezi ujao, ni Stuttgart na sio Bayern Munich itakayopepea bendera ya Ujerumani katika champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya.

 • Tarehe 26.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHba
 • Tarehe 26.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHba