VFB Stuttgart kutetea ubingwa ijumaa hii | Michezo | DW | 07.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

VFB Stuttgart kutetea ubingwa ijumaa hii

Msimu wa 2007/08 wa Bundesliga unaanza ijumaa hii pale mabingwa stuttgart wakiumana na makamo-bingwa Schalke.

Wakati Schalke imechoshwa na sifa za kumaliza makamo-bingwa,inataka mwaka huu wa 50 tangu kutwaa taji mara ya mwisho 1958,kuvaa tena taji-taji ambalo msimu uliopita walilipoteza siku ya mwisho ya msimu mikononi mwa Stuttgart.

Ijumaa hii Stuttgart, iko nyumbani ikiikaribisha Schalke na inadai jogoo la mjini halitaliwachia la shmba kuwika.

Ile hali ya msangao imepotea kwani mara hii mabingwa watetezi-Stuttgart ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kutwaa ubingwa.Msimu uliopita,timu hii chini ya kocha Armin Veh,ilitoka nyuma na kuzipiku Schalke na Bremen na mwishoe siku ya mwisho ya Ligi ikatoroka na kombe.Ikicheza na mastadi wapya na wachanga akina Mario Gomez na Roberto Hilbert.

Mara hii msangao unaweza ukazushwa na timu yoyote kuanzia Bayern munich,Schalke hadi timu zilizopanda daraja ya kwanza Karlsruhe na hata Hansa Rostock.

Kocha wa Stuttgart si mtu wa kutoa porojo na ameonya alivyosema, “Hatutaki kudai kwamba tunataka kutamba tena na kutetea taji letu.Tutaingia uwanjani msimu huu miguu chini.”

Stuttgart ilitwaA UBINGWA BAADA YA KUJENGA TIMU YENYE CHIPUKIZI WAPYA NA KUACHANA NA MAJINA MAKUBWA YA ZAMANI:

Haikuwa na fedha miezi 12 iliopita kununua wachezaji maarufu.Sasa wakiwa wamekata tiketi ya champion League-kombe la klabu bingwa-nafasi ambayo kikawaida huchukuliwa na Bayern Munich,Stuttghart ina hakika ya kuingioza vitita vya fedha.

Hatahivyo, wakati Munich imetumia euro milioni 70 kununua mastadi wapya kujiimarisha kwa msimu mpya, Stuttgart imetumia milioni 7 tu kumn unua mshambulizi wa kirumania Ciprian Marica; euro milioni 2.3 kwa kipa Raphael Schaefer na milioni 1.5 kwa mshambulizi wa ki-brazil Ewerthon .Stadi wa Uturuki Yildiray Basturk amejiunga bila malipo kutoka Hertha Berlin.

Wachezaji hao wapya wanajiunga na chipukizi wa zamani mfano wa Gomez lakini pia na wakongwe wenye maarifa kama Fernando Meira na Thomas Hitzspereger.

Kombe la klabu bingwa barani Ulaya-champions League,limewavutia wachezaji hao kujiounga na STUTTGART ILI NAO WAJITEMBEZE BARANI Ulaya:Hatahivyo, kucheza champions League na wakati huo huo kutetea taji lake katika Bundesliga ni kama kupanda farasi 2 na kuna hatari ya kuanguka.

Shabaha ya Stuttgart katika champions League,kwa muujibu wa meneja wake Heldt, ni kucheza katika duru ya pili alao.

Sherehe ya kufungua msimu mpya jumamosi iliopita huko Stuttgart, ilihudhuriwa na mashabiki 60,000-ishara kwamba alao mashabiki wanatarajia ushindi mwengine msimu huu ujao.Wazi ,Schalke,Bremen na Bayern Münich, hazitaipa mteremko.

Ikiwa siku njema huonekana alfajiri, keshokutwa ijumaa Stuttgart itapofungua dimba na Schalke itatuonesha.

 • Tarehe 07.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbS
 • Tarehe 07.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbS