1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VAR ni gumzo Uingereza yatengeneza au yaharibu?

Sekione Kitojo
11 Novemba 2019

VAR yageuka  kuwa  gumzo Uingereza, Liverpool yawalima mabingwa  watetezi Manchester City.

https://p.dw.com/p/3SqX7
Fußball Premier League Liverpool - Manchester City
Picha: picture-alliance/empics/P. Byrne

Katika  ligi  ya  England,  matumizi  ya  mfumo wa  kumsaidia  mwamuzi VAR katika  Premier League  umezua  tafarani  baada  ya  nia  ya  kumsaidia mwamuzi  kutoa  maamuzi  sahihi  na  haki  kwa  timu, umeingia  sasa katika mjadala  mkuu  iwapo ni  sasa  kuutumia  ama  la. Badala  ya  kuleta unafuu unaleta  hali ya mkorogano wa  maamuzi.

Fußball Champions League - Gruppe E - KRC Genk v Liverpool
Mo Salah na Sadio Mane wakifurahia bao kw timu yao ya Liverpool dhidi ya Man CityPicha: AFP/F. Walschaerts

Badala  ya  kuondoa  utata, maafisa  wa  VAR  na  marefa  wanaonekana kuzidisha  tatizo  badala  ya  kutatua kutokana  na  maamuzi  yao.

Mwishoni  mwa  juma  kulikuwa  na  maamuzi  kadhaa  ya  utata ,yakihusisha  bao  la  Sheffield United dhidi ya  Tottenham Hotspur siku  ya Jumamosi  na  pia  jana  katika  mchezo  wa  mafahali  wawili  Liverpool  na Manchester City.

Kuna mambo  kadhaa  ya  kiufundi  ambayo  yanaweza  kujadiliwa  baada ya  ushindi  wa  Liverpool wa  mabao 3-1  dhidi ya  Manchester City.

Kocha wa  Liverpool Juergen Klopp alisema  baada  ya  mchezo  huo:

Fußball Champions League - Gruppe E - KRC Genk v Liverpool
Kocha wa Liverpool Juergen Klopp akimpa mkono mshambuliaji wake Sadio Mane Picha: Reuters/P. Childs

"Naupenda  mchezo, napenda hali mchezoni, ilikuwa safi sana. Watu, walikuwa katika  hali ya  kushangaza. na hasa dhidi ya  wapinzani  imara. nilisiki  kila  mtu  akiniuliza kuhusu hilo. Sijaona  bado. Penalti ana kushika kwa mkono kabla ya Ferbinho  kufunga, kwa  hiyo siwezi  sema chochote juu  yake. Lakini  nilisikia ulikuwa  mkono wa Bernardo Silva, sijui, lakini naweza  kufikiria kuwa  sio hali  ambayo  Pep anaifurahia. Hiyo ni kawaida.

Kuna mengi ya  kujadili  katika  mchezo  huo  lakini  kulikuwa na kitu kimoja  dhahiri katika kikosi  cha  Juergen Klopp dhidi  ya  mabingwa watetezi ni  kimwili walikuwa na nguvu. katika  michezo  ambayo City inadhibiti mpira na  kuwakimbiza  wapinzani kwa pasi  zao za  kijanja, ilionekana  kimsingi ni  kwa  kiasi  gani  timu  yao  ilikuwa  ndogo lakini wakati Liverpool  inadhibiti  kikosi cha  Pep Guardiola kwa uwezo wa nguvu, ukosefu wao wa misuli ulionekana  dhahiri.  Katika  mchezo wa jana Pep Guardiola  amejifunza  jambo.

Champions League - FC Shakhtar Donetsk - Manchester City
Kocha wa Manchester City Pep GuardiolaPicha: picture-alliance/dpa/Ukrinform

"Nadhani  leo tumeonesha katika  uwanja  mgumu  kabisa  duniani sababu  kwanini  sisi  ni  mabingwa. Kwa hiyo , moja  kati  ya  mchezo mzuri  kabisa  tuliowahi  kuonesha nikiwa kama meneja  katika  wakati huu katika  uwanja  huu. Sina la  kusema. Bahati  mbaya  tumepoteza. Hongera Juergen  na  timu  yake  bora ya Liverpool  kushinda , 3-1. Nafikiri ulikuwa  mchezo  mzuri kwa  timu  zote, kwa  ajili  ya  Premier League, kwa  mabilioni  ya  watu ambao  waliuangalia  mchezo  huo."

Kocha wa  Liverpool Juergen Klopp  amesema  ni  mapema  mno kuzungumzia  juu  ya  ubingwa  wa  ligi na  mwenzake  wa  Manchester City Pep Guardiola  anaendelea  kujipa  moyo  licha  ya  kipigo.

Mshindi mara tatu  wa  taji la Premier mlinzi  Jonny Evans amechukua hatua  ya  kutuliza  mzuka wa  mashabiki  wa  Leicester City  kwamba klabu  hiyo  inaweza  kurudia  kile  ilichokifanya wakati waliponyakua taji hilo  mwaka  2016 akisema  kipindi cha  heka  heka  cha  wakati wa Krismas kitatoa  picha halisi  zaidi. Mlinzi  huyo mwenye umri  wa  miaka 31  kutoka  Ireland ya  kaskazini ambaye  ameshinda  mataji  matatu  ya ligi  akiwa  na  Manchester United, amekuwa  na  jukumu  muhimu  katika kikosi cha  Mbweha hao  msimu  huu  chini  ya  kocha  kutoka  Ireland pia Brendan Rodgers.