Uturuki ya kumbwa na visa vya rushwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 27.12.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Uturuki ya kumbwa na visa vya rushwa

Kufuatia misukosuko ya kuzidi kwa kashfa za rushwa zinazowakabili viongozi wa ngazi ya juu wa kiserikali nchini Uturuki, zimesababisha uongozi wa waziri mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan kutetereka.

Waziri mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan akielekea ofisini kwake mjini Ankara Uturuki

Waziri mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogan akielekea ofisini kwake mjini Ankara Uturuki

Kufuatia kashfa hiyo, Tayyip Erdogan amelazishwa kuwafukuza mawaziri wake watatu, ambapo mmoja wao alimhusisha waziri mkuu mwenyewe katika kashfa hiyo ya rushwa.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na mwendesha mkuu wa mashtaka wa serikali wa nchi hiyo, Muammer Akkas, kuwa Kumekuwa na mashinikizo kadhaa kutoka kwake na Mkuu wa Polisi wa nchi hiyo, wa kutaka watu wengine wakamatwe kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi, na kwamba mpaka sasa wanayo orodha ya viongozi kadhaa wa ngazi ya juu serikalini na wafanya biashara wakubwa wanaotuhumiwa kushiriki katika kashfa za kutoa hongo na rushwa zinazoitingisha serikali hiyo.

Waandamanaji nchini Uturuki wakidai uongozi wote wa serikali ujiuzulu

Waandamanaji nchini Uturuki wakidai uongozi wote wa serikali ujiuzulu

Madai hayo kutoka kwa mwendesha mashtaka mkuu wa serikali, yamekuja siku moja tu baada ya Waziri mkuu Erdogan kuwatimua mawaziri karibú nusu ya baraza zima la mawaziri, na kujiuzulu kwa waziri wa masuala ya uchumi na mazingira.

Waziri huyo aliyejiudhulu, Erdogana Bayraktar, alikiambia kituo cha televisheni cha NTV kuwa yeye, amelazimishwa kujiuzulu hivyo na anaamini kuwa hata waziri mkuu mwenyewe anapaswa kujiuzulu.

Hata hivyo waziri mkuu Erdogan alisema,anaamini kuwa yeye ndiye mlengwa mkuu wa kashfa hizo za rushwa zilizoibuka nchini mwake, lakini anaamini kuwa wote waliodhamiria mumchafua wataambulia patupu.

Wengi wa waangalizi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa rushwa imekomaa nchini uturuki, tangu Erdogan alipoingia madarakani, ambapo kumekuwa na misukosuko mingi ya hali ya kiuchumi na utawala wa kidikteta.

Waziri mkuu Edorgan mwenye umri wa miaka 59, ni kiongozi aliaminika kuingia madarakani na kuahidi kupambana vikali na vitendo vya rushwa na kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi ya nchi hiyo, ambaye amesaidia kuiifanya nchi hiyo iimarike kiuchumi.

Kashfa hizo ziliibuka tarehe 17 ya mwezi huu,polisi ya nchi hiyo ilipotangaza

Waziri wa masuala ya uchumi aliyejiuzulu Uturuki Zafer Caglayan kushoto

Waziri wa masuala ya uchumi aliyejiuzulu Uturuki Zafer Caglayan kushoto

operesheni ya msako wa vinara wa rushwa katika serikali hiyo, kufuatia fedha zilizokuwa zikivushwa kutoka nchini humo na kupelekwa Iran na ubadhirifu wa fedha za miradi kadhaa ya kiserikali, ambapo watu wengi walikamatwa, wakiwemo watoto wa mawaziri watatu wa nchi hiyo.

Misukosuko hiyo imesababisha kuyumba kwa soko la kibiashara la nchi hiyo na hata kuathirika na kushuka kwa thamani pesa ya nchi hiyo.

Waangalizi wengine wa masuala ya kisiasa nchini uturuki wanasema kuwa, kashfa hizo zinaweza kuathiri uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Machi mwaka ujao.

Mwandishi: Diana Kago
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com