1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Utawala wa kijeshi wa Burkinabe wavunja vyama vya siasa

30 Januari 2026

Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso umevivunja vyama vyote vya siasa nchini humo pamoja na kufuta sheria zinazosimamia vyama hivyo, hii ikiwa ni kulingana na amri iliyodhinishwa na serikali siku ya Alhamisi.

https://p.dw.com/p/57iXX
Burkina Faso | Rais wa mpito Ibrahim Traore
Rais wa mpito wa Burkina Faso Ibrahim Traore akiwa kwenye kikao cha mashauriano cha Jukwaa la Uchumi na Kibinadamu la Urusi-Afrika katika Kituo cha Maonyesho cha Mkutano na Maonyesho yaPicha: Stanislav Krasilnikov/ITAR-TASS/IMAGO

Waziri wa Mamlaka za Maeneo Emile Zerbo amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya mamlaka kugundua kwamba vyama hivyo vinakiuka miongozo ya kuanzishwa kwao, kusababisha migawanyiko miongoni mwa wananchi na kudhoofisha muundo wa kijamii.

Shughuli za vyama vya siasa kwa muda mrefu zimezuiwa chini ya utawala wa kijeshi na amri hiyo inataka mali za vyama hivyo kuhamishiwa serikalini, limearifu shirika la habari la serikali.

Wanaharakati wanasema hatua kama hizo zimelenga uhuru wa raia na upinzani tangu mamlaka ya kijeshi ilipochukua mamlaka katika mapinduzi ya 2022.