Usain Bolt aandika historia | Michezo | DW | 21.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Usain Bolt aandika historia

Mjamaica Bolt amenzakua medali zote 2 za dhahabu katika mita 100 na 200.

Natalie du Toit, muogoleaji kiwete/A.Kusini

Natalie du Toit, muogoleaji kiwete/A.Kusini

Mvua kali ilionyesha hii leo mjini Beijing,ilichelewesha mashindano ya riadha ya leo asubuhi . Wakati mashindano ya kutembea km 20 yalianza kwa wakati licha ya dharuba kali ya mvua,ale za kurusha mkuki zaliahirishwa hadi baadae.Mashindano za wanawake za kuruka juu/high/jump zamechelewa pia kuanya .

Wajamaica lakini, wanamshangiria Ragae boy Usain Bolt ,mwanariadha wa kwanza katika historia ya olimpik jana kunyakua mataji yote 2 ya mbio fupi mita 100 na 200 na rekodi za dunia katika historia ya miaka 112 ya ya olimpik.

Kufuatia ushundi wake wa ajabu kabisa wa mbio ya mita 200 hapo jana ,mjamaica Usain Bolt sio tu amejipatia binafsi medali yake za pili za dhahabu,bali halkadhalika amekuwa mwanariadha wa kwanya katika historia za miaka 112 za olimpik kushinda mbio yote 2 /mita 100 na 200.

Muda wake wa sek.19.30 ni rekodi mpza za dunia na hivyo umeifuta ile rekodi za masafa hazo za mita 200 za muamerika Michael Johnson alioiweka august mosi,1996 katika micheyo za Atlanta.

Kwahivzo, Usain Bolt ni mwanadamu wa kwanza tangu Carl Lewis wa Marekani katika michezo ya Los Angeles, 1984 na wa 9 kwa jumla kushinda mita 100 na 200 katika michezo ile ile ya Olimpik.

Usain Bolt halkadhalika ni mwanariadha wapili kutoka Jamaica kushinda medali za dhahabu za mita 200 baada za mtanguliyi wake Don Quarrie,huko Montreal,1976.

Wasichana wa Jamaica nao si wadogo wamedhihirisha kama kikosi chao cha wanaume wana mkuki mjarabu unaowaumiya wamarekani.

Leo wamarekani 3 wanapambana na wajamaica 3 katika kinyan|ganyiro cha mbio ya mita 200 wanawake.Wajamaica wakiongoywa na bingwa wao wa mita 100 Shelly/Ann Fraser,wanakusudia kuyoa tena medali yote 3/dhahabu,fedha na shaba kama walivzofanza katika mita 100.

Kenza baada za kukosa medali za dhahabu na kuondokea na ile za fedha katika mita 1.500 sasa inalenga kutamba katika mita 5000 wanaume na wanawake pamoja na mita 800 wanaume hapo jumamosi kabla mbio ya marathon ya wanaume jumapili hii/siku za mwisho za michezo za Beijing.

Wenyeji China wangali wakiongoza wazi katika orodha za medali wakiwa na jumla ya medali 45 ya dhahabu,15 ya fedha na 21 za shaba kwa 27 tu za dhahabu za Marekani.

Uingereza sasa imenyakua nafasi za 3 huku Ujerumani ikiangukia nafasi za 6 kwa medali 11 za dhahabu, 8 za fedha na 10 ya shaba /jumla 29.

Miongoni mwa nchi ya kiafrika yiliyonzakua dhahabu/usoni kabisa ni Kenya na Ethiopia,Zimbabwe na Kamerun.