1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi: Tumezuia shambulizi la Ukraine katika mpaka wa kusini

1 Juni 2023

Urusi imesema imezuia jaribio la uvamizi wa Ukraine kupitia mpaka wake wa kusini katika jimbo la Belgorod.

https://p.dw.com/p/4S4TC
Russland Evakuierung von Kindern aus der Region Belgorod
Picha: Mikhail Tokmakov/TASS/dpa/picture alliance

Wizara ya ulinzi mjini Moscow imesema jeshi la Urusi limetumia ndege na mizinga kuwazuia wanajeshi wa Ukraine kuingia katika ardhi ya Urusi.

Mkoa wa Belgorod umeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara mnamo siku za hivi karibuni, yakiwemo makubwa yaliyodumu kwa siku mbili wiki jana.

Soma pia: Eneo la mpakani kati ya Urusi na Ukraine laendelea kuwa tete

Mkuu wa mkoa huo, Vyacheslav Gladkov amesema mamia ya watu wamefurika katika kituo cha wasio na makaazi, wakikimbia mashambulizi.

 Hayo yanajiri baada ya Urusi kufanya mashambulizi mengine dhidi ya mji mkuu wa Ukraine, Kiev, ambayo yameuawa watu watatu usiku wa kuamkia leo. Jeshi la anga la Ukraine limesema limeyaharibu makombora yote kumi yaliyofyatuliwa na Urusi.