1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yasema imezima jaribio dhidi ya daraja la Crimea

2 Septemba 2023

Urusi imesema leo kuwa imeziharibu boti tatu za Ukraine zinazoendeshwa kwa rimoti zilizojaribu kulishambulia daraja muhimu linaloiunganisha Urusi na rasi ya Crimea.

https://p.dw.com/p/4Vsoi
Krim Kerch Brücke
Daraja kwenye mlango bahari wa Kerch unaoiunganisha Urusi na Rasi ya CrimeaPicha: AA/picture alliance

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema moja ya droni hizo za majini iliharibiwa jana Ijumaa na nyingine mbili mapema leo asubuhi katika operesheni iliyolazimisha daraja hilo kufungwa kwa muda ikiwa ni mara ya tatu chini ya kipindi cha mwaka mmoja.

Ukraine haijasema chochote kuhusu madai hayo yaliyotolewa na Moscow

Daraja hilo kwenye ujia wa maji wa Kerch ni kiungo muhimu kwa usambazaji wa mahitaji ya vikosi vya Urusi vinavyopiga vitani nchini Ukraine.

Tangu Moscow ilipotuma vikosi vyake nchini Ukraine, kumekuwa na majaribio kadhaa ya kuliharibu daraja hilo ikiwemo shambulizi la mwezi Oktoba mwaka jana lilosababisha vifo vya watu watatu.