1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yafanya mashambulizi mapya ya anga mjini Kiev

30 Mei 2023

Urusi imefanya wimbi jipya la mashambulizi katika mji mkuu wa Kiev mapema leo Jumanne huku milio ya ving'ora ikisika katika maeneo kadhaa ya Ukraine kama tahadhari.

https://p.dw.com/p/4RxOR
Ukraine Kiew | Russicher Drohnen-Angriff
Picha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Meya wa mji mkuu huo Vitali Klitschko ameandika katika mtandao wa Telegram juu ya mashambulizi hayo ya anga huku akiwataka wakaazi wa mji huo kutotoka nje.

Klitschko ameongeza kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 27 amekimbizwa hospitali baada ya kupata majeraha kusini magharibi mwa wilaya ya Holosiivskyi.

Soma pia: Urusi yafanya mashambulio mapya dhidi ya Ukraine

Maafisa wa utawala wa kijeshi mjini Kiev wamesema mifumo yao ya ulinzi iko imara na kwamba inazuia mashambulizi hayo.

Mashambulizi ya leo Jumanne yalikuwa ni ya 17 yaliyoulenga mji mkuu Kiev mwezi huu pekee, na yametokea baada ya Urusi kufanya mashambulizi kama hayo jana Jumatatu ikiwemo shambulio moja la mchana.