Upigaji kura waanza Thailand | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.02.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Upigaji kura waanza Thailand

Raia wa Thailand wanapiga kura leo Jumapili(02.02.2014)chini ya ulinzi mkali katika uchaguzi ambao unaweza kuitumbukiza nchi hiyo iliyogawika katika mzozo mkubwa zaidi wa kisiasa.

Thailand Wahlen Wahllokale

Zoezi la upigaji kura limeanza

Mzozo huo wa kisiasa utasababisha mshindi kushindwa kufanyakazi kwa miezi kadhaa kutokana na maandamano ya mitaani, kesi mahakamani na mivutano bungeni.

Zoezi la upigaji kura lilianza kwa amani siku moja baada ya watu saba kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na miripuko wakati wa mapambano kati ya waungaji mkono na wapinzani wa waziri mkuu Yingluck Shinawatra katika eneo la kaskazini la mji mkuu Bangkok ambalo ni ngome kuu ya chama chake cha Puea Thai.

Thailand Bangkok Proteste Wahl Anti Regierung 1.2.14

Waandamanaji wakionesha upinzani wao dhidi ya upigaji kura

Upigaji kura ulisitishwa katika wilaya na baadhi ya vituo vingine vya upigaji kura vilishindwa kufunguliwa kwasababu ya mbinyo kutoka kwa waandamanaji wanaoipinga serikali. Upigaji kura nje ya mji mkuu na upande wa kusini haukuathirika.

"Hali kwa jumla ni shwari na hatujapokea ripoti zozote za ghasia asubuhi ya leo," mkuu wa baraza la usalama la taifa Paradorn Pattanatabutr ameliambia shirika la habari la Reuters. "Waandamanaji wanafanya maandamano kwa amani kuonesha upinzani wao dhidi ya uchaguzi huo."

Wapiga kura wana hofu

Mabango ya kawaida kwa ajili ya kampeni , na picha kubwa na hali ya shauku ya uchaguzi havionekani , pamoja na mamilioni ya wapiga kura ambao wanahofu ya kutokea ghasia ama wanaelemea kupinga zoezi hilo la uchaguzi lenye lengo la kuurejesha tena madarakani uongozi wa kisiasa unaodhibitiwa na kaka yake waziri mkuu Yingluck ambaye ni tajiri mkubwa, Thaksin Shinawatra.

Demonstrationen in Bangkok

Waandanamaji wakipinga zoezi la kupiga kura

Thaksin, mwenye umri wa miaka 64, anapendwa na kuogopewa nchini Thailand, lakini vyama vyake vimeshinda kila uchaguzi tangu mwaka 2001. Wapinzani wake wanasema kuwa ni bepari mpenda rushwa ambaye anatawala kwa kumtumia dada yake wakati yeye binafsi akiwa uhamishoni nchini Dubai.

Kuna haja ya mabadiliko

"Hatuzuwii uchaguzi. Tunauahirisha tu," amesema Nipon Kaewsook, mwenye umri wa miaka 42, mmoja katika ya mamia ya waandamanaji wanaozuwia ofisi ya wilaya ya Ratchathewi katikati ya mji mkuu Bangkok wakizuwia usambazaji wa makasha ya karatasi za kupigia kura.

"Bado tunahitaji uchaguzi, lakini tunahitaji kwanza mabadiliko ," ameongeza Nipon, mwalimu wa lugha ya kiingereza kutoka Phattalung kusini mwa Thailand.

Waandamanaji waliimba "Yingluck achia ngazi" na "Thaksin afungwe"! Wameondoa picha zilizokuwa zimewekwa mbele ya masanduku ya kura na kuzipeleka katika eneo la kuegesha magari nyuma ya jengo.

Sherehe za ushindi za Yingluck huenda zikawa za chini chini tu.

Thailand Bangkok Proteste Wahl Anti Regierung 1.2.14

Waandamanaji katika mitaa ya mjini Bangkok

Katika wakati ambapo viti bungeni havitaweza kukamilika, anaweza kujikuta katika hali ngumu, akikabiliwa na kesi mahakamani na kutoshindwa kupitisha miswada na bajeti muhimu ya kufufua uchumi ambao unayumba.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Caro Robi

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com