Umwagikaji damu bado unaendelea nchini Iraq. | Matukio ya Kisiasa | DW | 13.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Umwagikaji damu bado unaendelea nchini Iraq.

watu 18 wameuwawa na wengine 40 kujeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kuliripua gari karibu na chuo cha mjini Baghdad magharibi mwa Iraq

Leo hii nchini Iraq mashambulio kadhaa ya mabomu yametokea katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo kuanzia huko Baghdad ambapo watu 18 wameuwawa baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kuliripua gari.

Bomu jingine kali kabisa liliripuka katika eneo la kati la mji wa Baghdad ambapo watu 16 waliuwawa huku polisi wakijaribu kurudisha hali ya usalama.

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliripua gari lililokuwa limesheheni mabomu nje ya bohari la chakula magharibi mwa mji mkuu Baghdad na kuharibu nyumba na kuwajeruhi watu wasiopungua 40 waliokuwa wamesimama karibu na mahala hapo.

Mashambulio yamekuwa yakifanyaka usiku kucha katika maeneo ya kusini mwa mji Baghdad ambapo watu wane waliuwawa na wanamgambo na wapiganaji katika eneo la Suwaib.

Mauaji hayo yametokea licha ya kuwepo opresheni ya usalama inayofanywa na wanajeshi wa Marekani na Iraq ikiwa ni siku moja baada ya mfululizo wa mashambulio ya mabomu katika maeneo ya masoko ambapo watu kiasi 79 waliuwawa na wengine 165 kupelekwa.

Katika eneo la Mansur karibu na mahala palipotokea shambulio la bomu hii leo kuliwekwa vizuizi vya hali ya juu vya polisi lakini pamoja na hilo wengi wa wairaqi wametoa masikitiko yao juu ya kutokea mashambulio ya mabomu.

Hapo jana waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki akitoa hotuba kupitia televisheni aliwataka wairaqkuunga mkono kupelekwa maelfu ya wanajeshi na polisi nchini humo lakini sasa wananchi wairaq wanasema mambo yanaonyesha kurudi kinyumenyume kwani pamoja na kuongezwa kwa idadi ya polisi na majeshi ya kulinda amani wairaqi hali kila uchao inazidi kuwapotezea matumaini.Hali imekuwa mbaya na maji yamezidi unga.

Nasser al Ani mbunge wa kisunni anasema mpango wa amani nchini Iraq hauwezi kufanya kazi kwasababu kosa limeshafanyika tangu Marekani ilipoamua kuuangusha utawala wa Saddam Hussein.

Ameongeza kusema mbunge huyo kwamba kosa kubwa lililofanywa ni kulivunja jeshi la Iraq.

Huku hali ikiendelea kuwa mbaya zaidi huko Iraq kansela Angela Merkel wa Ujerumani akizungumza mbele ya bunge la ulaya hii leo amesema kwamba Umoja wa Ulaya,pamoja na Marekani na Urussi lazima zifanye juhudi katika mpango wa amani ambao utaiweka Iraq katika hali ya usalama na kumaliza vita.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com