1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umwagaji damu wapunguwa Iraq

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYEm

BAGHDAD

Akitaja kushuka kwa asilimia 60 machafuko ya umwagaji damu nchini Iraq katika kipindi cha miezi sita iliopita Generali David Petreaus wa Marekani amesema leo hii kwamba kudumisha usalama ni rashisi zaidi kuliko kuanzisha usalama na kwamba hali hiyo inampa nafasi ya kuweza kufanya maamuzi kwa kuendana na hali.

Petreaus amesema mashambulizi ya kila wiki na vifo vya raia nchini Iraq vimeshuka kufikia viwango ambavyo havikuwahi kushuhudiwa tokea mapema mwaka 2006.

Amesema kupunguwa kwa umwagaji damu huo kunampa nafasi ya kufanya marekebisho ya vikosi kukabiliana na matatizo yaliobakia kwenye maeneo mengine likiwemo la kaskazini.