Umoja wa Ulaya kujadili kuhusu Uhamiaji | Matukio ya Kisiasa | DW | 12.07.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Umoja wa Ulaya kujadili kuhusu Uhamiaji

Mawaziri wa Mambo ya Ndani ya mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakutana nchini Austria kuhusu mzozo wa wakimbizi barani Ulaya, Ujerumani, Italia na Austria zikipanga kushirikiana kwa karibu ili kutatua tatizo hilo.

Hayo ni kwa mujibu wa mawaziri wa masuala ya ndani ya mataifa hayo matatu kwenye mkutano uliofanyika katika mkesha wa mkutano rasmi hivi leo, suala hilo tata ambalo linazidi kuyagawa mataifa ya Umoja wa Ulaya.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Horst Seehofer alisema kuwa anatarajia kufikia makubaliano na Italia ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kuhusu suala tata la kuwarejesha nchini humo wahamiaji kutoka Ujerumani. Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano na mwenzake wa Italia Matteo Salvini, Seehofer alisema maafisa kutoka nchi hizo mbili watakutana haraka iwezekenavyo kulijadili suala hilo.

Suala tata la wahamiaji

"Baada ya mazungumzo ya Vienna na kansela Sebastian Kurz na mwnzangu Kickl na baada ya majadiliano ya jana na mwezangu Salvini, ninamatumaini kuwa tunaweza kufaulu kwa pamoja kusuluhisha hili suala la uhamiaji wa wakimbizi.” Alisema Seehorfer. 

Lakini mwenzake wa Italia, Matteo Salvini, amelitupilia mbali pendekezo hilo, akisema kinachotakiwa kwanza ni kuwepo kwa mkakati mpana zaidi wa kulinda mipaka ya Ulaya. Salvini, ambaye kama alivyo Seehofer ana msimamo mkali kuhusu uhamiaji hadi kufikia kiwango cha kuvutana na viongozi wa dini nchini mwake, amesema hayo walipokutana na Seehorfer kabla ya mkutano wa kilele usio rasmi wa mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya baadaye hii leo.

Österreich Innsbruck - EU-Innenminister | Matteo Salvini, Italien & Horst Seehofer, Deutschland (DW/B. Riegert)

Mateo Salvini wa Italia kushota na Horst Seefer wa Ujerumani

Salvini alisema wazi kuwa anatarajia kuona hatua zaidi za kuimarisha mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya kabla ya kukubaliana na mpango wowote wa kuwachukua tena wahamiaji.

Shinikizo za kumtaka Seehorfer ajiuzulu

Seehorfer, pia amejikuta katika wakati mgumu kutokana na matamshi yake ya dhihaka dhidi ya wahamiaji, ikiwa ni pamoja na matamshi aliyoyatoa katika siku yake ya kuzaliwa kwamba alikuwa anatimiza miaka 69, na wahamiaji 69 walikuwa wakirejeshwa nchini Afghanistan. Mmoja wa wahamiaji hao, Jamal Nasser Mamoudi alijiua, muda mfupi baada ya kurejeshwa, kisa kilichoibua miito kutoka vyama vya upinzani vya hapa Ujerumani vikimtaka Seehorfer kujiuzulu.  

Flüchtlinge im Mittelmeer gerettet (picture alliance/dpa/Bunde3swehr/Gotschalk)

Wahamiaji wanaokolewa wakijaribu kuingia barani Ulaya.

Viongozi wanaopinga uhamiaji wa chama maarufu cha mrengo wa kulia cha AFD, hawakutoa maoni yao mara moja kuhusu suala hilo. Aidha viongozi wakuu wa chama cha Angela Merkel cha CDU ama hata kansela Merkel mwenyewe hajazungumzia suala hilo.

Leo jioni Seehofer anatarajiwa kushinda na mawaziri wa haki na masuala ya ndani kutoka mataifa ya Umoja wa Ulaya, jijini Innsbruck, Austria. Huenda hatua hiyo ikapunguza joto la matamshi yake na mmoja wa watu ambao wanahusishwa moja kwa moja na sera zake. Lakini ni bayana kuwa Seerhofer amekuwa mzigo katika serikali ya Angela Merkel na siku zake za kusimamia wizara zinahasibika sasa.

 

Mwandishi: Shisia Wasilwa, Ap, Dpa

Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com