1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yasema Urusi yashambulia meli ya nafaka

9 Novemba 2023

Ukraine imesema Urusi imeifyatulia kombora meli ya kiraia iliyokuwa ikiingia bandarini katika eneo la Bahari Nyeusi la Odesa.

https://p.dw.com/p/4Yaha
Ukraine imesema Urusi imeshambulia meli ya kiraia iliyokuwa inaingia katika bandari ya Bahari Nyeusi kwenye eneo la Odessa
Ukraine imesema Urusi imeshambulia meli ya kiraia iliyokuwa inaingia katika bandari ya Bahari Nyeusi kwenye eneo la OdessaPicha: Presidential Office of Ukraine/SvenSimon/picture alliance

Shambulizi hilo lilimuua nahodha wa meli na kuwajeruhi watumishi wengine wa meli hiyo.

Taarifa ya jeshi la Ukraine imesema kupitia mtandao wa Telegram imesema watumishi watatu, raia wa Ufilipino, walijeruhiwa na mmoja wao amelazwa.

Moscow haijasema chochote kuhusiana na taarifa hizo.

Mwezi Julai, Urusi ilijiondoa kwenye makubaliano ya usafirishaji salama wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi, kutoka kwenye bandari za Ukraine, ambayo baadae ilianzisha njia za muda ili kuendeleza mchakato huo.