Ujerumani kukata tikiti ya kombe la dunia
11 Oktoba 2013Hata matokeo ya sare yataiwezesha timu hiyo kushiriki fainali hizo kwa kutegemea matokeo ya mechi nyengine kwenye kundi lao ambalo lina timu za Austria, Sweden, Kazakhstan, jamhuri ya Ireland, Ujerumani na visiwa vya Faroe.
Katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya kufanyika kwa mchezo huo ,kocha wa timu ya Ujerumani, Joachim Löw, amethibitisha kwamba kikosi chake cha kwanza cha wachezaji 10 kiko imara isipokuwa mchezaji mmoja wa kiungo upande wa kushoto, Marco Reus, ambaye ni majeruhi pamoja na mchezaji mzoevu wa timu ya taifa, Lukas Podolski.
Wakati huo huo mchezaji chipukizi wa Uingereza Daniel Sturridge atakuwamo katika kikosi cha "Simba watatu " usiku huu kupambana na Montenegro katika uwanja wa Wembley baada ya kukosa mchezo wa kwanza mwezi uliopita dhidi ya Moldova kutokana na maumivu.
Sturridge ataungana na Wayne Rooney katika ushambuliaji baada ya kukosekana nae katika mchezo uliopita dhidi ya Moldova kutokana na maumivu.