1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani bado ina kazi kubwa ya kupambana na Ufisadi

Amina Mjahid
25 Januari 2022

Shirika la kimataifa la kupambana na ufisadi Transparency International limetoa ripoti yake iliyo na pande mbili, kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi. Ujerumani inaendelea kushikilia nafasi yake ya 10 katika vita hivyo.

https://p.dw.com/p/463fu
Symbolbild Geschäftsmann
Picha: Arno Burgi/dpa/picture alliance

Ujerumani imekuwa ikishikilia nafasi hiyo kwa mara ya nne mfululizo ndani ya miaka minne ya ripoti ya shirika hilo la kimataifa la kupambana na ufisadi duniani Transparency International (CPI) ikiwa na alama 80 kati ya 100.

Denmark, New Zealand na Finland zilichukua nafasi za juu kwa mara nyengine tena kama mataifa yanayoangaliwa kuwa na viwango vya chini vya rushwa zikiwa na alama 88, kwenye mizani ambayo 0 ina maana ni fisadi mkubwa na 100 ina maana nchi isiyo na ufisadi kabisa. Syria, Sudan na Somalia ndizo zimevuta mkia kama nchi zinazoongoza kwa ufisadi.

Shirika hilo limesema alama inayotolewa kwa mataifa tofauti ndio muhimu hata kuliko nafasi inayowekwa inayoweza kubadilika kutokana na idadi ya mataifa na maeneo yanayotathiminiwa na CPI. Kwa mwaka 2021 serikali 180 ziliingia katika orodha hiyo.

Matokeo ya Ujerumani yanayonesha namna ilivyojitahidi kuondoa rushwa katika sekta zake za umma, na yanayonesha namna sheria zake zinavyoendelea kufanikiwa kudhibiti matendo ya ufisadi kama matumizi mabaya ya madaraka, hongo na wizi wa mali ya umma. Hilo bila shaka lilitarajiwa kwa taifa hilo lililojijengea demokrasia, lililo na tasisi imara na linalozingatia utawala wa sheria.

Australia imeshuka kwa pointi 4 katika mapambano dhidi ya rushwa

ASEAN Summit 2021 I Scott Morrison I Australien
Waziri Mkuu wa Australia Scott MorrisonPicha: Lukas Coch/AAP/imago images

Marekani iliyo na alama 67 imeingia katika nafasi ya 27 katika orodha hiyo ikifuatiwa na Hong Kong, Canada,  Austria, Ufaransa, Ubelgiji na Australia zote zikiwa chini ya Ujerumani. Kukaa juu katika orodha hiyo ni bora kuliko kuvuta mkia. Ausralia imeshuka kwa pointi 4 kuanzia mwaka jana na Kwa ujerumani kubakia katika nafasi yake ya 80 kunamaanisha haijaweka juhudi za kutosha kushughulia changamoto zilizoko katika mapambano dhidi ya ufisadi.

Hartmut Bäumer Mwenyekiti wa shirika hilo upande wa Ujerumani amesema kupitia taarifa yake kwamba bado kuna mapungufu makubwa katika kila upande wa jamii na ujerumani haijafika mbali kukabiliana na tatizo hilo, akitoa  mfano wa kisa kikubwa kilichotokea mwaka uliopita kilichosababisha wabunge wawili wa kihfidhina kujiuzulu baada ya kugunduliwa kuwa walitumia nguvu zao kisiasa kujipatia fedha takriban dola milioni 2.3 katika mpango wa kununua barakoa wakati wa janga la corona. Baadae Mahakama moja ya Munich haikuwakuta na hatia ikisema madai dhidi yaohayakukidhi viwango vya kisheria vya ujerumani vya rushwa.

Ndio maana Bäumer anasema sheria dhidi ya tatizo hili zinapaswa kuangaliwa upya na kuimarishwa.

Chanzo: DW Page