1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza na Italia zapanga kuanza ligi zao

Deo Kaji Makomba
29 Mei 2020

Wakati janga la virusi vya Corona likiendelea kuitesa dunia, nchi za Uingereza na Italia zimepanga kuanzisha tena ligi zao za soka wakati ligi kuu ya soka ya Ujerumani, Bundesliga tayari ilikwishaanza.

https://p.dw.com/p/3czEw
BG Kandidaten Deutscher Fußballbotschafter | Pascal Gross
Picha: Imago-Images/PA Images/M. Kerton

Ifuatayo ni hali ya ligi kuu tano za soka barani Ulaya na zingine na vikombe hasa katika wakati huu wa wa mlipuko wa janga la virusi vya Corona.

Tukianzia hapa nchini Ujerumani ni kwamba ligi kuu ya soka nchini humu, Bundesliga, ilianza kutimua vumbi tena hapo Mei 16 baada ya kusimamishwa kwa muda wa miezi miwili kwa mechi tisa za mwisho na mechi zote sasa zikipigwa huku milango ya viwanja ikifungwa kutoruhusu watazamaji kuingia uwanjani na chini ya mashariti ya kanuni kali za usafi ili kuepusha uwezekano wa kuenea kwa maambukizi mapya ya virusi vya Corona. Klabu ya Bayern Munich iko kileleni mwa ligi hiyo kwa kuwa na tofauti ya alama saba dhidi ya wapinzani wao wa karibu katika msimamo wa ligi kuu hiyo huku hai matumaini ya kutetea ubingwa wake kwa mara ya nane mfululizo. Ligi hiyo ya Bundesliga inatarajiwa kufikia tamati hapo tarehe 27 mwezi Juni na final ya kikombe itachezwa itapigwa tarehe 4 Julai baada ya mechi za nusu fainali hapo Juni 9 na Juni 10.

ENGLAND

Nako nchini Uingereza vilabu vya soka nchini humo vimekubaliana kwa muda kuanza tena kwa ligi kuu ya soka nchini humo kuanzia Juni 17, kwa michezo miwili mikononi na raundi 10 zilizosalia kuchezwa, ikiripotiwa kufikia tamati kufikia Julai 25. Mechi zote zitachezwa huku milango ya viwanja ikifungwa ili kutokuruhusu watazamaji kuingia uwanjani. Vilabu hivyo vya soka pia  vilikubaliana kuanza tena mazoezi ya pamoja. Maamuzi ya kuendelea mbele na mchakato wa kuanza tena kwa ligi hiyo yatatolewa na serikali ya nchi hiyo pindi mahitaji yote ya kiusalama yatakapotekelezwa. Klabu ya kandanda ya Liverpool ina alama 25 kibindoni na ikishikilia usukani wa ligi hiyo ikifuatiwa na Manchester City na inaweza kulitwaa taji la ligi hiyo kama itashinda mechi yake ya kwanza na City kupotea mchezo wake.

UHISPANIA
Kule nchini Hispania serikali ya nchi hiyo imeeuhusu ligi kuu ya soka nchini humo La liga kuanza tena kuanzia tarehe 28 mwezi Juni na kuendelea chini ya sheria kali ya kanuni za afya na mechi zote zikipigwa bila ya watazamaji uwanjani. Kipute cha kwanza kinatarajiwa kupigwa Juni 12 na raundi 11 zilizosalia kuchezwa na inarifiwa kuwa mechi zimepangwa kuchezwa kila siku. Vigogo wa soka nchini humo Barcelona wako kileleni kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya wapinzani wao Real Madrid. Fainali kati ya timu mbili zinazotokea jimbo la Basque nchini Uhispania, Athletic Bilbao na Real Sociedad huenda ikaahirishwa hadi mwaka ujao katika jitihada za kuhakikisha uwanja unajaa mashabiki.

ITALIA

Nayo serikali ya Italia imeipatia ligi kuu ya soka nchini humo taa ya kijani kama ishara ya kuanza kutika tena kwa kivumbi cha ligi hiyo Juni 20. Kuna raundi 12 zilizosalaia kuchezwa, na mechi zote zitachezwa  katika viwanja tupu bila ya kuwa na watazamaji. Vilabu vya soka nchini humo vililirejea katika mazoezi yao na pia mazoezi ya pamoja yaliruhusiwa tena. Kombe la Italia linaweza kutangulia kuanza kwa mchezo wa ligi mnamo Juni 13 na fainali siku nne za mwisho baadaye. Mabingwa watetezi Juventus wanakalia kigoda cha ligi hiyo wakiwa mbele ya alama moja dhidi ya Lazio wanaoshililia nafasi ya pili kwa kuwa na alama 62 kibindoni.

UFARANSA
Kule nchini Ufaransa ligi ya soka nchini humo maarufu kama Ligue 1 ili ilifutwa na vinara wa ligi hiyo Paris Saint German walitangaza mabingwa  mnamo tarehe 39 mwezi Aprili baada ya serikali ya nchi hiyo kupiga marufuku matukio ya michezo ya kulipwa ndani ya nchi hiyo hadi Agost 31 mwaka huu.

Kwingineko, Uholanzi iliipiga teke ligi yake na hakuna bingwa aliyetangazwa. Ligi ya Ubelgiji pia haikuanzishwa tena na vinara wa ligi hiyo Club Brugge walitawazwa kuwa  mabingwa wakati kombe la fainali litachezwa Agosti 1. Vinara Celtic walitangazwa mabingwa wa Scotland katika msimu wao uliofutwa. Austria ilianza tena michezo ya fainali ya kombe lake Ijumaa na michezo ya ligi kufuata Jumanne. Denmark imeanza tena na mashabiki wa kweli. Swedwen inatarajiwa kuanza msimu wa ligi yake mnamo Juni 14. Hungary ambayo tayari imeanza tena ligi yake huku  ikiruhusu baadhi ya mashabiki kuingia uwanjani chini ya uangalizi mkali wa mashabiki kutokusogeleana. Kama vile Serbia ambao wanaanza tena mechi zao mwishoni mwa wiki. na Urusi imepanga kucheza tena kuanzia mwezi Juni 21.

Nchini Ufaransa, Paris Saint German walitangaza mabingwa mnamo tarehe 39 mwezi Aprili
Nchini Ufaransa, Paris Saint German walitangaza mabingwa mnamo tarehe 39 mwezi ApriliPicha: Getty Images/AFP/S. Schurmann
Italia imeruhusu ligi kuu nchini humo kuanza tena Juni 20
Italia imeruhusu ligi kuu nchini humo kuanza tena Juni 20Picha: picture-alliance/Sportphoto24/M. Ozbot
Katika ligi ya Laliga ya Uhispania, kipute cha kwanza kinatarajiwa kupigwa Juni 12
Katika ligi ya Laliga ya Uhispania, kipute cha kwanza kinatarajiwa kupigwa Juni 12Picha: imago images/Cordon Press/Miguelez Sports

Chanzo: dpa