Uhuru wa habari wazidi kutishiwa Afrika ya kati | Matukio ya Afrika | DW | 03.05.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Uhuru wa habari wazidi kutishiwa Afrika ya kati

Licha ya uongozi mpya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuahidi kulinda uhuru wa vyombo vya habari baada ya kuuangusha utawala wa rais Francois Bozize, hali inaelezwa kuwa mbaya kuliko ilivyokuwa chini ya Bozize.

Burundian journalists march in the streets of Burundi's capital Bujumbura on May 03, 2011. Hundreds of journalist joined the march to mark the International day of the freedom of the press and called for the release of a fellow journalist, Jean-Claude Kavumbagu, who was arrested by the Burundian authorities and accused of treason for having doubted the Burundian governments ability to prevent a Somali Islamist insurgents attack on Burundian soil. The prosecutor in the case is asking for life imprisonment as punishment for the journalist's offense. Burundi is one of the two countries who have provided soldiers to the African Union's military force helping to uphold the Somali transitional government. Slogan translates as 'Freedom of the Press. Where are we? Where are we going?' AFP PHOTO/ESDRAS NDIKUMANA (Photo credit should read Esdras Ndikumana/AFP/Getty Images)

Burundi Pressefreiheit

Zaidi ya mwezi mmoja uliopita, waasi katika Jamhuri ya Afrika ya kati waliuangusha utawala wa dikteta Francois Bozize. Wakiwa chini ya shinikizo kutoka mataifa jirani, kulifanyika majadiliano, ambapo muungano wa waasi wa SELEKA uliunda serikali ya mpito kwa kushirikiana na maafisa kutoka utawala uliopita, upinzani na mashirika ya kiraia. Kiongozi wa waasi Michel Djotodia aliteuiliwa kuwa rais mpya.

Waasi wa Seleka wakilinda doria mjini Bangui baada ya kuuangusha utawala wa Francois Bizize.

Waasi wa Seleka wakilinda doria mjini Bangui baada ya kuuangusha utawala wa Francois Bizize.

Ni matumaini yaliyopotea

Chini ya utawala wa Bozize, uhuru wa habari ulikandamizwa kwa kiasi kikubwa. Waandishi wa habari walishtakiwa, kukamatwa ovyo au hata kutoweka. Kuondolewa kwa Bozize kulitoa matumaini mapya, wakati kiongozi mpya alipoahidi uhuru zaidi wa habari. Hata hivyo, waandishi wameendelea kutishiwa hata na watawala wapya. Ndiyo maana waandishi hao walifanya maandamano ya amani.

Katika redio yoyote unayofungulia, unaskia tu sauti kutoka vipaza sauti katika Texi inayofanya kazi zake katika mji wa Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Hilo sio jambo la kawaida. Kituo bora zaid cha redio - Ndeke Lika ni maarufu kwa habari mototo, mijadala ya kisiasa na uhariri motomoto. Lakini leo hii yote hayo hayapo tena. Unasikia ujumbe tu unaorudiwa mara kwa mara na mtangazaji.

"Vyombo vya habari katika Jamhuri ya Afrika ya Kati vinaporwa. Usalama wa waandishi wa habari unazidi kutishiwa kila siku, na uhuru wa kujieleza na maoni haudhaminiwi na serikali. Tunaviomba vyombo vya kimataifa vitusaidie kuripoti kuhusu hali ya uhuru wa mawazo katika nchi yetu iliyosahaulika", anasema mtangazi mmoja wa redio Ndeke Lika.

Kiongozi mpya wa Jamhuri ya Afrika ya kati Michel Djotodia

Kiongozi mpya wa Jamhuri ya Afrika ya kati Michel Djotodia

Wito wa maandamano ya amani

Redio hiyo imeitikia wito wa shirikisho la waandishi wa habari katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wa kufanyika kwa maandamano ya nchi nzima. Siku ya leo, waandishi wote wanapaswa kususia kazi zao kwa siku moja. Vituo vya redio hucheza tu muziki aina ya Dudel sambamba na matangazo ya maandamano. Magazeti machache ya Jamhuri ya Afrika ya Kati pia hayaonekani leo. Kwa upande wa Televisheni ambayo haijalishi kutoka na kukatika mara kwa umeme, zinaonyeshwa tu makala za zamani.

Licha ya kususia kazi, waandishi wa kituo cha redio cha Ndeke Lika wamehudhuria mkutano wa asubuhi. Kituo hicho kiko katika jengo dogo lililoko ndani ya uwanja uliozungukwa na ukuta mrefu. katika mlango wa kuingilia wapo wanajeshi wawili wenye silaha, lakini haijulakini iwapo wako pale kwa ajili ya kulinda au kudhibiti kituo hicho. Mhariri mkuu wa redio hiyo Jean Claude Ali Syhlas anasema wapo hapo karibi kila siku.

Lakini hata kabla ya waasi kuuteka mji mkuu wa bangui, serikali iliyokuwa madarakani, iliwachochea vijana kuharibi mtambo wa kurushia amatangazo wa redio hiyo, lakini hawakufanikiwa katika azma yao hiyo. Tarehe 24 Machi wasi wa Seleka waliuvamia mji mkuu na kuangusha utawala wa Bozize. Siku iliyofuata, waasi hao walikivamia kituo hicho cha redio kwa mara ya kwanza.

Rais aliyepinduliwa Francois Bozize

Rais aliyepinduliwa Francois Bozize

Mambo ni yaleyale

"Walikuja wakatuambia: Chukuweni tahadhari, vinginevyo tutawamaliza. Hapa sisi hatuna ulinzi wowote - ingawa viongozi wa waasi walituahidi kutulinda, katika hali ya angalia unachokisema, sisi hatuwezi kujihesabu kuwa tunalindwa. Hata kama raia wa kawaida, tumekuwa tukitishiwa. Nyumba ya mwenzetu mmoja iliporowa. Tunapata masaibu makubwa chini ya waasi kuliko ilivyokuwa chini ya utawala wa Bozize. Kwa sababu hawazungumzi lugha yetu. Kwa mfano, walikuja wakachuku skrin ya computer wakidhani ni TV. Waliiba rimoti ya kiyoyozi wakidhani ni simu. Hawajasoma, na lugha yao ni vurugu tu. Hata kama rais anatuhakikishia uhuru wa vyombo vya habari, lakini watu wake hawawezi kutulinda", alisema Syhlas akiwaelezea wanajeshi wa Seleka.

Hata viongozi wa waasi ambao ni wasomi hawaelewi vizuri jukumu la vyombo vy ahabari. Na hiyo inafanya kazi ya vyombo huru kama redio Ndeke Lika kuwa ngumu sana. Kituo hiki kinapata ufadhili wake kutoka nje, katika nchi za Ufaransa na Ubelgji, na kutoka Umoja wa Ulaya. Jamhuri ya Afrika ya kati ni nchi maskini sana na iliyokithiri kwa rushwa kiasi cha kufanya vigumu kwa kituo huru cha redio kuendesha shughuli zake.

Wafuasi wa kiongozi mpya Michel Djotodia wakiandamana mjini Bangui kuonyesha mshikamano na utawala mpya.

Wafuasi wa kiongozi mpya Michel Djotodia wakiandamana mjini Bangui kuonyesha mshikamano na utawala mpya.

Mapambano yanaendelea

Lakini hivi sasa vyombo vy ahabari vina jukumu kubwa, anasema mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari cha haki za binaadamu, ambacho ni mmoja ya vyama muhimu zaidi visivyo vya kiserikali nchini Jamhuri ya Afrika ya kati. "Kazi ya vyombo vya habari ni kuwapa imani raia, na kuionyesha serikali mpya, kuwa haiwezi kutawala bila watu. Waasi kweli wamekuja kutawala nchi, lakini raia wanateseka," alisema Mkurugenzi huyo ambaye hakutana jina lake litajwe kwa sababu za usalama.

Ndiyo maana haishangazi leo hii kuona waandishi wa habari katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wakionyesha ujasiri na kuitisha maandamano, hata kama maandamano hayo ni ya tahadhari na kimya.

Mwandishi: Schlindwein Simone/Iddi Ismail Ssessanga
Mhariri: Daniel Gakuba