1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUhispania

Uhispania yafanya uchaguzi muhimu wa serikali za mitaa

28 Mei 2023

Wapiga kura nchini Uhispania wanateremka vituoni leo kwa uchaguzi wa tawala za majimbo na majiji ambao matokeo yake yatakuwa kipimo kwa uchaguzi mkuu wa baadaye mwishoni mwa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4Ruib
Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez akipiga kura katika uchaguzi wa majimbo
Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez akipiga kura katika uchaguzi wa majimboPicha: Juan Medina/REUTERS

Upigaji kura unafanyika kwenye majimbo 12 pamoja na miji na manispaa 8,000 ambayo idadi kubwa inaongozwa hivi sasa na chama tawala cha kisoshalisti cha PSOE.

Kura za maoni ya umma zimebashiri chama cha kihafidhina cha People Party (PP) kitaimarisha ngome yake kwenye uchaguzi wa leo.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa tangu saa tatu asubuhi na vitafungwa saa mbili usiku. Mchuano unatazamiwa kuwa mkali kwenye maeneo mengi ambayo vyama hivyo viwili havina udhibiti wa moja kwa moja ikiwemo mkoa wa Valencia. 

Hata hivyo kwenye jimbo la Madrid uliko mji mkuu, mwanasiasa wa upinzani Isabel Diaz Ayuso anatazamiwa kushinda muhula mwingine madarakani.