Uhamiaji - Hakuna njia ya kuingia Peponi | Noa Bongo | DW | 21.05.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Noa Bongo

Uhamiaji - Hakuna njia ya kuingia Peponi

Bara la Afrika limo mbioni. Mamilioni ya wakaazi wake hulihama bara hilo kutafuta maisha bora katika mabara mengine au kutoroka vita na migogoro isiyokoma. Wengi huwa na ndoto ya kuwa na maisha bora barani Ulaya.

Bara la Afrika limo mbioni. Lakini safari inaweza kuwa hatari

Bara la Afrika limo mbioni. Lakini safari inaweza kuwa hatari

Bobby ni miongoni mwa wahamiaji milioni 17. Ndio taswira kamili ya idadi ya wahamiaji kutoka barani Afrika kulingana na shirika la kimataifa kuhusu wahamiaji. Lakini hata hivyo wengi hubakia barani humu kwa matumaini ya kupata ajira katika mashamba ya kakao Magharibi mwa Afrika au viwandani nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo Bobby, aliamua kuihama nchi yake ya Ghana na kupiga kambi nchini Ujerumani. Lakini kumbe Ujerumani si peponi kama alivyodhania. Maisha ni magumu hasa kupata kibali cha kuishi nchini humo na pia kutafuta kazi itakayomletea pato la kukimu mahitaji yake.

Katika mfululizo wa vipindi vyetu kuhusu uhamiaji tunachunguza suala la uhamiaji na kukutana na wahamiaji kutoka kote barani Afrika. Na pia kuchunguza njia hatari zinazotumiwa na wahamiaji hawa kuingia barani Ulaya. Hapa tunakutana na vijana wawili kutoka Afrika ambao hatimaye wanaamua kurudi nyumbani baada ya maisha kuwa magumu zaidi barani Ulaya, na pia hadithi ya raia mmoja wa Urejumani aliyehamia nchini Uganda katika juhudi za kutafuta maisha bora.

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘Noa bongo Jenga Maisha yako; vinasikika katika lugha; Kingereza, Kifaransa, Kiswahili, Hausa, Kireno na Amharic. Na vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni nchini Ujerumani

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa