​​​​​​​Ugua pole Fergie | Michezo | DW | 07.05.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

​​​​​​​Ugua pole Fergie

Klabu ya Manchester United imewashukuru wapenzi wa kandanda waliotuma salamu za kumtakia nafuu ya haraka kocha mkongwe Alex Ferguson kufuatia upasuaji wa dharura uliotokana na kuvuja damu kwenye ubongo

United haijatoa taarifa yoyote mpya kuhusiana na hali ya Ferguson, tangu iliposema kuwa upasuaji uliofanywa Jumamosi ulifanikiwa lakini bado yuko chumba cha wagonjwa mahututi ili kurejea katika hali ya kawaida.

Miongoni mwa waliotuma salamu za kheri ni makocha Arsene Wenger, Pep Guardiola, Antonio Conte na Jurgen Klopp ambao walizungumza namna wanavyomuenzi Ferguson. Klopp alisema "Nilikutana na Sir Alex baada ya mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Rome, alinipita pamoja na Gerrard na tukasema maneno machache naye na wakati niliskia jana niliwa njiani kwenda London sikuamini kuwa kitu kama hicho kinaweza kutokea. Lakini kinaweza kutokea kwetu sote hivyo nnamuombea kwa asilimia 100 na namtakia kila la kheri yeye na familia yake. Atakuwa sawa tena nna uhakika kuhusu hilo na ningependa tena kumuona".

Hapo jana, mabingwa wa Ligi ya Premier msimu huu Manchester City walibeba kombe lao rasmi huku Pep Guardiola akiongeza taji jingine la ligi kwa yale aliyopata Uhispania na Ujerumani. Hongereni sana mashabiki wa Man City. Msimu ujao maadui watazidi kuwa wengi

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com