1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugomvi wa wazazi na athari za kisaikolojia kwa watoto

8 Agosti 2013

Mamilioni ya watoto duniani ni wahanga wa ugomvi uliomo majumbani mwao pale wazazi wao wanapopitia kipindi cha migogoro ya kifamilia na wanasaikolojia wanasema hilo hubakia muda mrefu akilini mwa watoto hao.

https://p.dw.com/p/19LxE
Gewalt gegen Kinder nimmt zu, Jugendämter Deutschland #38266064 - fear © Firma V
Symbolbild Gewalt gegen KinderPicha: Fotolia/Firma V

Ulevi, usaliti, hali ngumu ya maisha na tabia ya kiburi vinatajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vya migogoro ya majumbani na ambayo husababisha watoto kupoteza mapenzi kwa wazazi wao na hata kujenga tabia ya kisasi, ambayo nayo inaweza kuja kuwaathiri watoto wao watakapokuwa watu wazima.

Ambatana na Hashim Gulana kwenye makala hii ya Mbiu ya Mnyonge kujifunza mengi juu ya kadhia hii inayoweza kuepukwa na hivyo kuwasaidia watoto kupitisha utoto wao kwa salama.

Makala: Hashim Gulana
Mhariri: Mohammed Khelef