Ugaidi wakutanisha Mawaziri wa ulaya Brussels | Matukio ya Kisiasa | DW | 20.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ugaidi wakutanisha Mawaziri wa ulaya Brussels

Mawaziri wa Mambo ya Ndani na wale wa sheria wa Umoja wa Ulaya leo hii wanafanya mkutano wa dharura wenye lengo la kuzidisha ulinzi katika maeneo ya mipaka yake baada ya kuuwawa kwa kiongozi wa mashambulizi ya Paris.

Belgien Frankreich Innenminister Bernard Cazeneuve in Brüssel

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve na Waziri wa Sheria Christiane Taubira mjini Brussels

Abdelhamid Abaaoud, raia wa Ubeligiji mwinye asili ya Morocco, anatuhumiwa kuwa muhusika aliyepanga mashambilizi ambayo yalisababisha watu 129 wapoteze maisha, kwa niaba ya kundi la Dola la Kiislamu, aliuwawa jana kutokana na shambulio la polisi katika jengo moja huko kaskazini mwa jiji la Paris.

Kuna fikra kwamba kijana huyo wa umri wa miaka 28 alikuwa nchini Syria, ambako alipata uwezo wa kupanga mashambulizi dhidi ya mataifa ya Magharibi. Kwa hivyo uwepo wake nchini Ufaransa unaongeza unazusha maswali kuhusu namna Ulaya inavyoshughulikia mgogoro mkubwa kabisa wa kikanda wa wimbi la wahamiaji tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Kauli ya mawaziri wa mambo ya mambo ya ndani

Frankreich Saint Denis Polizei Absperrung Terrorismus

Eneo tete la Saint Denis mjini Paris

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema taifa lake halijapata taarifa yoyote ya onyo kutoka mataifa wanachama kwamba Abaaoud yupo katika maeneo ya kanda hiyo, na kupasawa kanda hiyo kuwa macho mara moja, kujipanga na kujilinda dhidi ya kitisho cha ugaidi.

Akiwasikili katika eneo la mkutano, nae wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Theresa May alinikuliwa akisema "Ningalipenda kuona mataifa yote wanachama, wanajikita katika kuboresha hatua na adhabu kwa wote wenye kuhusika na usafirishaji haramu wa binaadamu na silaha, na majina ya abiria yahifadhiwe katika kumbukumbu. Tunahitaji maendeleo ya hatua hiyo haraka, mazungumzo yamechukua muda mrefu, yanapaswa kufikiwa hitimisho".

Mawaziri wa mambo ya ndani na wa sheria watajadili namna ya kuhimarisha ukaguzi katika maeneo ya mipaka kwa wasafiri wote katika mataifa 26 yaliyo katika umoja wa Schengen kama hatua za dharura.

Kitisho cha wakimbizi

Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Vals alisema baadhi ya wauwaji wa mkasa wa Paris walichukulia kigezo cha mgogoro wa uhamiaji barani Ulaya kuingia katika eneo hilo pasipo kubainika na kuonya mataifa yaliyo ukanda wa Schengen, kwamba yanaweza kuwa katika hatari endapo hayatodhibiti ulinzi katika mipaka yake.

Abaaoud inamuungano na Syria na kandoni mwa mwili wake kulikutwa pasiposi ya Syria ya mshambuliaji mmoja ambae jambo lilizusha wasiwasi kwamba mipiganiaji huyo wa vita vya jihadi aliingia Ulaya kwa kigezo cha ukimbizi katika taifa hilo lililigubikwa na vita, kwa lengo la kupanga njama za kufanya mashambulizi.

Nchini Marekani, Bunge lililogubikwa na chama cha Republican, walipiga kura ya kupiga marufuku wakimbizi wa Syria na Iraq kuingia Marekani mpaka hatua madhubuti za ukaguzi zitakapoimarishwa. Na Urusi yenyewe bado ipo katika tafakari baada ya mkasa wa ndege yake ya abiria kudunguliwa nchini Misri na kusababisha vifo vya watu wote 224 walikuwemo katika ndege hiyo, katika shambulizi lingine linalodaiwa kufanywa na kundi la Dola la Kiislamu. Mabaraza yote mawili ya bunge la taifa hilo yatafanya mikutano mkubwa leo hii ya kujadili namna ya kukabiliana na ugaidi.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com