Udhibiti wa jiji la Manchester wadhihirika | Michezo | DW | 20.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Udhibiti wa jiji la Manchester wadhihirika

Katika upande wa samawati, Pep Guardiola ananawiri mwanzoni mwa taaluma yake katika klabu ya Manchester City baada ya kushinda mechi tano kati ya tano katika Premier League

Katika upande mwekundu, Jose Mourinho anagundua masaibu waliyopitia David Moyes na Louis van Gaal wakati wakijaribu kufikia mafanikio aliyopata Alex Ferguson wakati wa uongozi wake wa miaka 26 katika klabu ya Manchester United.

Baada ya kuanza msimu kwa ushindi wa mechi tatu mfululizo, United sasa wamepoteza mechi tatu mfululizo katika kipindi cha karibu wiki moja. Hapo jana walizabwa tatu moja na Watford na Mourinho anasema huenda hali hiyo inatokana na baadhi ya wachezaji wake kuzidiwa na shinikizo

"Nilifahamu kikamilifu kuwa timu yetu sio bora zaidi. Kwamba tulikuwa na wachezaji wengi ambao hawajakamilika na wanaweza kufanya makosa. Shaka niliyonayo ni namna tunaweza kupambana na hali ngumu kwa sababu matokeo mabaya kawaida hutokea mara kwa mara. Lakini nahisi baadhi ya wachezaji huenda wanahisi shinikizo kubwa na jukumu walilo nalo. Nahisi kwa mtazamo wa pamoja, nna mambo mazuri tu ya kusema kuwahusu". alisema Jose.

United tayari wako nyuma ya viongozi City na pengo la pointi sita. Tottenham iliwafunga Sunderland moja bila na kusonga katika nafasi ya tatu nyuma ya everton inayoshikilia nafasi ya pili. Arsenal, Chelsea na Liverpool zinakamilisha sita bora zote zikiwa na pointi 10.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com