SiasaUkraine
Uchunguzi: Putin huenda alitoa Kombora lililoangusha ndege
8 Februari 2023
Matangazo
Wakitaja mawasiliano ya simu yaliyonaswa, wachunguzi wamesema kuna dalili kubwa kuwa Putin aliidhinisha binafsi kusafirishwa kwa kombora hilo hadi kwa wanaharakati wanaopigania kujitenga wakiungwa mkono na Urusi wakati wa mapigano mashariki mwa Ukraine mwaka wa 2014.
Lakini uchunguzi huo umesitishwa kwa sababu uchunguzi wote umefanyika kwa kina kuhusu kudunguliwa kwa ndege hiyo, ambayo iliwauwa watu wote 298 waliokuwemo.
Tangazo hilo limejiri chini ya miezi mitatu baada ya mahakama ya Uholanzi kuwahukumu Warusi wawili na mmoja wa Ukraine kwa kuwauwa wote waliokuwemo kwenye ndege ya Malaysia MH17, baada ya kuwashitaki bila ya wao kuwepo mahakamani.