1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUswisi

UBS yainunua benki pinzani ya Credit Suisse kutuliza masoko

20 Machi 2023

Benki ya UBS imeinunua benki pinzani ya mikopo inayokumbwa na matatizo ya Credit Suisse kwa kitita cha dola bilioni 3.24. Hii ni kufuatia mazungumzo ya dharura kuizuia benki hiyo kuchochea mgogoro wa kimataifa wa benki

https://p.dw.com/p/4Ov6T
Schweiz Zürich | Logos von Credit Suisse und UBS
Picha: Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

Benki ya UBS imeinunua benki pinzani ya mikopo inayokumbwa na matatizo ya Credit Suisse kwa kitita cha dola bilioni 3.24. Hii ni kufuatia mazungumzo ya dharura hapo jana ya kuizuia benki hiyo kuchochea mgogoro mpana wa kimataifa wa benki.

Serikali ya Uswisi imesema mpango huo, ambao benki kubwa kabisa nchini humo itainunua benki ya pili kwa ukubwa, ni muhimu ili kuepusha mtikisiko wa kiuchumi kusambaa kote nchini na nje ya nchi.

Hatua hiyo imekaribishwa na serikali za Marekani, Umoja wa Ulaya na Uingereza ambazo zimesema itasaidia kurejesha utulivu wa kifedha, baada ya wiki ya msukosuko kufuatia kuanguka kwa benki mbili za Marekani. Credit Suisse ilipewa dola bilioni 54 na benki kuu ya Uswisi wiki hii kama fedha za kuinusuru.

Katika taarifa Benki kuu ya Uswisi ilisema "suluhisho limepatikana ili kupata uthabiti wa kifedha na kulinda uchumi wa Uswizi katika hali hii ya kipekee"