1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Prof. Ibrahim Noor Sharif wa Chuo Kikuu cha Qaboos, Oman.
Prof. Ibrahim Noor Sharif wa Chuo Kikuu cha Qaboos, Oman.Picha: DW/M. Khelef

Ubantu na ukrioli wa Kiswahili

Mohammed Khelef
27 Agosti 2014

Ingawa nadharia pekee inayosomeshwa vyuoni ni kwamba Kiswahili ni Kibantu kwa asili na kwa dhati yake, bado kuna hoja inayosema kwamba asili ya lugha hii ya upwa wa Afrika ya Mashariki ni mchanganyiko.

https://p.dw.com/p/1D2kA

Katika sehemu hii ya mfululizo wa makala za Kiswahili Kina Wenyewe, Mohammed Khelef anazungumza na mtafiti na mtaalamu wa Sanaa na Lugha kutoka Chuo Kikuu cha Qaboos nchini Oman, Profesa Ibrahim Noor Sharif, ambaye anahoji kwamba Kiswahili kilichopo sasa kimeanza kutumika karne ya 16 baada ya ujio wa Wabantu kwenye eneo la mashariki mwa Afrika, na sio kabla ya hapo.

Kusikiliza makala nzima, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Saumu Yusuf