Tuzo ya Nobel ya Uchumi yaenda kwa Wamarekani | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.10.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Tuzo ya Nobel ya Uchumi yaenda kwa Wamarekani

Wataalamu wawili wa Kimarekani kuhusu masuala ya uchumi wameshinda Tuzo ya Nobel ya Uchumi ya mwaka huu, kwa kujumuisha ubunifu na mazingira katika ukuaji wa kiuchumi.

Jopo la tuzo hiyo limesema wanauchumi hao, William Nordhaus ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Yale na Paul Romer, aliyekuwa mkuu wa masuala ya uchumi katika Benki ya Dunia na sasa ni mhadhiri katika Chuo cha Biashara mjini New York, wameweza kuyapatia jibu maswali magumu ya wakati huu, juu ya namna ya kutengeneza uchumi endelevu na wa muda mrefu.

Jopo hilo limeongeza kuwa watu hao wawili wamepanua upeo wa uchambuzi wa kiuchumi, wakifafanua vyema namna uchumi wa masoko unavyoingiliana na mazingira asilia na ujuzi wa watu.

Wote wawili, Nordhaus na Romer, wamekuwa wakitajwa kwa muda mrefu kama wastahiki wa tuzo hiyo. Tuzo hiyo inaambatana na kitita cha Dola milioni moja.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com