Turnesh Dibaba atamba katika mita 5000. | Michezo | DW | 22.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Turnesh Dibaba atamba katika mita 5000.

ilikua tena leo siku ya Turnesh Dibaba kunyakua medali ya dhahabu katika mita 5000.kama alivyofanya katika mita 10.000

Turnesh Dibaba wa Ethiopia, ametamba tena katika mbio za mita 5000 hivi punde kama alivyotamba katika mita 10.000 wanawake.Hivyo, ameipatia Ethiopia medali yake ya 3 ya dhahabu kabla kesho mwenzake wa kiume Kenenisa Bekele kumuigiza katika finali ya mita 5000 wanaume atakapopambana na mkenya bingwa wa dunia Eluid kipochoge.Wajamaika wamenyakua medali nyengine ya dhahabu katika mita 100X leo wakiongozwa na bingwa wa rekodi ya dunia Usain Bolt.

Kesho pia ni finali ya mita 800 wanaume Kenya ikiweka matumaini kwa bingwa wake Winfried Bungei na binggwa wake wa dunia .

Katika dimba la olimpkk kabla ya finali ya kesho ya kukata na shoka kati ya Argentina na Nigeria, Brazil iliikomea leo Ubelgiji huko Shanghai mabao 3:0 na hivyo kutwaa medali ya shaba badala ya ile ya dhahabu iliotamani .Hata timu yake ya wasichana ikiwa na mastadi kama marta na Christiana iliondokea na medali ya fedha ilipokomewa jana kwa msangao wa wengi na Marekani bao 1:0.Ndoto ya Brazil kutawazwa mabingwa wa Olimpik kama katika kombe la dunia kwahivyo haikutimilia.

Afrika inatumai mabingwa wao wa olimpik huko Atlanta,1996 Nigeria, watatamba kesho mbele ya Argentina.

Mbrazil Maurren Higa Maggi lakini alitoroka leo na medali ya dhahabu katika long jump.

Michezo ya 29 ya olimpik ya Beijing ikikaribia kumalizika hapo jumapili tena kwa vishindo kama ilivyoanza, wenyeji China wanaongoza wazi katika orodha ya medali:

China ina jumla ya medali 46 za dhahabu,15 za fedha na 23 za shaba-jumla 84.

Marekani inafuata nafasi ya pili ikiwa na medali 30 za dhahabu, 36 za fedha na 35 za shaba-jumla 101.Ujerumani imeangukia nafasi ya 5 nyuma ya Uingereza na Russia.

Baada ya ushindi wa leo wa turnesh dibaba katika mita 5000, ethiopia imeshaipiku Kenya na hivyo inaongoza barani Afrika kwa medali zake 3 za dhahabu,ikifuatwa na Kenya.Uamuzi utakua kesho nani anatamba katika mita 5000,1500 na mita 800.

.