1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya kuchunguza chanzo cha ajali ya meli yatangazwa.

24 Septemba 2018

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza tume ya kuchunguza ajali ya kivuko cha MV Nyerere yenye wajumbe saba ambayo itaongozwa na Jenerali mstaafu, George Waitara. Tangazo hilo amelitoa kijijini Busya katika kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza leo, kufuatia mkasa wa kuzama kwa meli ambapo zaidi ya watu 217 wamepoteza maisha.

https://p.dw.com/p/35PJ4