Tsunami yaua wengi Indonesia. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 27.10.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Tsunami yaua wengi Indonesia.

Watu 112 wamefariki dunia na wengine zaidi ya mia tano hawajulikani walipo, baada ya kimbunga cha tsunami kukikumba kisiwa cha Mentawai, kilichoko kilomita 150 magharibi mwa pwani ya Sumatra nchini Indonesia.

default

Mlima Merapi nchini Indonesia, ambao volcano ililipuka.

Kimbuka hicho cha tsunami iliyofikia urefu wa mita tatu, kimekuja dakika chache baada ya tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo siku ya Jumatatu.

Nyumba kadhaa zimeharibiwa kutokana na mawimbi hayo yaliyofika mita 600 katika nchi kavu.

Indonesien Vulkanausbruch Merapi

Wanavijiji walioyahama makaazi yao, kutokana na kulipuka kwa volcano katika mlima Merapi.

Wakati huohuo watu 25 wamekufa baada ya mlima Merapi nchini Indonesia kulipuka mara tatu jana.

Hatua hiyo ilisababisha, maelfu ya watu kuyahama makaazi yao.

 • Tarehe 27.10.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza(ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Poj4
 • Tarehe 27.10.2010
 • Mwandishi Halima Nyanza(ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Poj4
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com