1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump amshambulia kwa maneno mwendesha mashtaka

5 Aprili 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amemshambulia mwendesha mashitaka wa New York Alvin Bragg kwa kufungua mashitaka ya uhalifu dhidi yake.

https://p.dw.com/p/4PiVm
USA | New York | Ex-Präsident Donald Trump
Rais Donald Trump wa Marekani akiwasili kutoa hotuba kwa wafuasi wake baada ya kutoka mahakamaniPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Trump amejitangaza kuwa mwathiriwa wa kuingiliwa uchaguzi bila kutolewa ushahidi wowote.

Akiwahutubia wafuasi waliokusanyika nyumbani kwake Mar-a-Lago katika mji wa Palm Beach, Florida, Trump amesema hakuwahi kudhani kitu kama kilichoshuhudiwa jana kingefanyika Marekani.

Awali, Trump mwenye umri wa miaka 76 alikanusha mashitaka yote 34 katika Mahakama ya Manhattan ya kughushi nyaraka za kibiashara, wakati waendesha mashitaka wakimtuhumu kwa kupanga malipo kwa wanawake wawili kabla ya uchaguzi wa 2016 ili kuzuia uchapishwaji wa taarifa za kuwa na mahusiano ya kingono naye.