Transperency Int.na rushua | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Transperency Int.na rushua

Desemba 9-siku ya kupiga vita rushua duniani.

"Wataje na uwaibishe"- ndicho chombo barabara cha kutumika ikiwa haki za raia zihifadhiwe.Shirka linalopigana na rushua ulimwenguni-TRANSPARENCY INTERNATIONAL- linatumia chombo hicho kupiga vita rushua na hata siku ya leo Desemba 9-siku ya kupiga vita rushua duniani.

Desemba 9 siku kama leo ni siku iliotangazwa na Umoja wa Mataifa ya kupambana na rushua.Ni siku inayotolewa orodha ya nchi zote ambazo makampuni na viwanda hutoa rushua.Kufichuliwa orodha ya nchi hizo huzianika hadharani zionekane na kuzuwia rushua kwa njia hiyo.

Si zamani sana rushua ikionekana madhambi madogo huku wanaokula wakidai "ikiwa hatutachukua rushua,wengine watachukua na wao ndio watakaofanya biashara."

Peter Eigen, muasisi wa Transparency International-shirika linalopiga vita rushua anasema.

" Tukichukua mfano tu wa serikali ya Ujerumani, haikujua ifanye je.Ilisema ikiwa kila pembe ya dunia kunatolewa rushua ,hatuwezi nasi kufumba mikono tu,kwani kufanya hivyo, tutapoteza miakataba ya biashara kila pahala."

Peter Eigen aliunda 1993 shirika hili la kupiga vita rushua-Transparency International .Mtumishi huyo wa zamani wa Banki kuu ya dunia ,alijumuika pamoja na viongozi wa kisiasa wa Afrika,Asia na Amerika kusini pamoja na watumishi wa Banki kuu ya dunia .Tangu wakati huo shirika hili lenye matawi yake mjini London na Berlin limegeuka chombo chenye m amlaka ya kupiga vita rushua na hongo.Peter Eigen ameamua kuunda shirika hilo kutokana na maarifa yake ya muda mrefu aliojipatia alipolitumikia Banki Kuu ya Dunia na hata barani Afrika.

"Kuna mradi wsa kujengwa bwawa ,kwengine mradi wa bomba la mafuta,njia za reli,bandari na miradi yote hiyo ina thamani ya mabilioni -miradi ambayo mwishoe haimfaidii mtu wakati miradi ya nafuu zaidi na ya dharura kama ujenzi wa shule na mahospitali inapuuzwa."

Uamuzi wa kuamua miradi kama hiyo huwa na matokeo yake ya kisiasa ambayo huathiri jamii nzima anaongeza kusemas Bw.Peter Eigen.

Kula rushua daima kunatokana na mikono 2-anatoa na anaepokea.Utaratibu huu ndio shasbaha ya Peter Eigen iliomfanya kuunda TRANSPERENCY INTERNATIONAL na amefanikiwa.Kwani, 1999, Ujerumani na nchi nyengine 34 zilitia saini mkataba wa kupinga rushua .Na sasa hata makampuni yanayobidi kulipa rushua nchi za nje yaweza kuadhbiwa yakitoa rushua.

Kuna mfano wa karibuni wa kisa kama hicho nchini Ujerumani:Kampuni la Siemen inavuma lilitoa rushua ya Euro milioni 1.5 .

Leo hii Peter Eigen ni mwenyekiti wa shirika jipya lililoundwa la EITI-Executive Industries Transperency Initiative" ambalo hjukumu lake kupiga vita rushua hasa katika nchi tajiri kwa mali ghafi.Kwani, nchi zenye utajiri wa mali ghafi ndiko rushua hunona.

Kwa Bw.Peter Eigen na shirika lake jipya la EITI hatua ya kwanza imechukuliwa katika vita vya kupambana na rushua kwa njia ya kutaja majina ya wanaotoa rushua.Lakini si kila kwa mara mkakati huo unafanikiwa-anadai rais wa zamani wa Botswana:Festus Mogae.Kwani, nchi yake ya Botswana inahesabnika kuwa miongoni mwa zile ziliopo usoni kabisa barani Afrika katika kuweka wazi hazikubaliani na rushua.

Lakini hii yawezekana tu-asema Mogae,pakiwepo serikali ya kidemokrasi yenye kuendesha shughuli zake kwa uwazi.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com