TOLUOSE : Airbus hatarini kupunguza wafanyakazi 10,000 | Habari za Ulimwengu | DW | 20.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TOLUOSE : Airbus hatarini kupunguza wafanyakazi 10,000

Kampuni ya ndege ya Airbus imeahirisha tangazo lake kuu juu ya upunguzaji wa ajira lililopangwa kutolewa leo hii.

Taarifa hii inafuatia mkutano wa shirika mama la kampuni ya Airbus la EADS katika mji wa Tolouse nchini Ufaransa ambapo bodi ya shirika hilo inasemekana kuwa imeshindwa kuweka saini mipango ya kuiunda upya kampuni hiyo. Baadhi ya repoti zinadokeza kwamba mageuzi ya kampuni hiyo ya Airbus yanaweza kusababisha kupunguza wafanyakazi 10,000 katika kampuni hiyo.

Jambo hili limepelekea mvutano wa kisiasa kati ya Ufaransa na Ujerumani kuhusiana na upunguzaji huo wa ajira unaotarajiwa.

EADS ilianza kuchunguza hatua za kubana matumizi za kampuni yake hiyo ya Airbus mwaka jana baada ya kujulikana kwamba kucheleweshwa kuwasilishwa kwa ndege aina ya jet super jumbo A380 kunaweza kukaugharimu muungano wa kampuni hiyo euro bilioni tano.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com