1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Togo yasogeza mbele uchaguzi wa bunge

10 Aprili 2024

Togo imeupeleka mbele uchaguzi wa bunge, kutokana na majadiliano makali yaliyozuka juu ya mabadiliko ya katiba. Taarifa iliyotolewa na serikali imesema uchaguzi huo utafanyika tarehe 29 Aprili.

https://p.dw.com/p/4ebDQ
Togo
Uchaguzi wa bunge Togo sasa utafanyika tarehe 29 mwezi Aprili Picha: AP

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, sababu ya kuahirishwa uchaguzi huo ni kutowa nafasi ya majadliano zaidi juu ya mageuzi yanayohitajika kufanyika kwenye katiba, hatua ambayo wapinzani wanasema ni mbinu ya kumpa nafasi Rais Faure Gnassibe kuendelea kusalia madarakani.

Upinzani Togo waitisha maandamano kupinga kuahirishwa uchaguzi wa Bunge

Kiongozi huyo ametawala tangu mwaka 2005 baada ya kumrithi baba yake, ambaye naye alikuwa ametawala kwa zaidi ya miongo mitatu.

Tamko la jana la serikali lilitoka siku chache kabla ya maandamano makubwa yaliyopangwa kufanywa na vyama vya upinzani.