1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTogo

Togo yapitisha katiba mpya inayorefusha muhula wa rais

26 Machi 2024

Togo imeikubali katiba mpya inayourefusha muhula wa rais kwa mwaka mmoja huku ikiweka kikwazo cha muhula wa rais kuwa mmoja pekee.

https://p.dw.com/p/4e9D5
Rais wa Togo Faure Gnassingbe
Rais wa Togo Faure GnassingbePicha: Ute Grabowsky/photothek/IMAGO

Hatua hii huenda ikamkubalia Rais Faure Gnassingbe kurefusha utawala wake wa miaka 19 kwa mwaka mmoja, kinyume na ilivyotarajiwa awali.

Chini ya katiba hii mpya ambayo haizingatii muda ambao Gnassingbe amekuwa madarakani tayari, Faure Ganssingbe sasa anaweza kuendelea kuwa madarakani hadi mwaka 2031, iwapo atachaguliwa tena mwakani. Uwezekano wa kuchaguliwa kwake tena ni mkubwa kwa kuwa chama chake ndicho kilicho na wingi bungeni.

Katiba hiyo mpya iliyopitishwa na wabunge 89 kati ya 91, inasema rais anachaguliwa na bunge kwa muhula mmoja wa miaka 6. Urais wa nchi hiyo ndogo yenye madini ya fosfati, umekuwa suala la kifamilia tangu mwaka 1967, pale Gnassingbe Eyadema alipochukua madaraka katika mapinduzi. Mwanawe alimrithi baada ya kifo chake 2005.