Tiger bado ni mahiri
15 Aprili 2019Hii ni mara ya tano Tiger kuvikwa koti la kijani ambalo ni ishara ya mchezaji ambaye ni bingwa wa shindano hilo.
Tiger amepitia kipindi kigumu kabla kuebuka mshindi tena kwani miaka michache iliyopita alikuwa amekata tamaa ya kuucheza tena mchezo huo baada ya kufanyiwa upasuaji na pia kuathirika na mambo ya kinyumbani.
"Mashindano haya yamekuwa muhimu sana kwangu kwa miaka mingi iliyopita. Nilikuwa na mashaka makubwa baada ya yaliyotokea miaka kadhaa iliyopita, nilikuwa siwezi kutembea, siwezi kuketi, sikuweza kulala, yani sikuweza kufanya chochote," alisema Tiger. "Yote yaliyofanyika leo, kulikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa na nafasi ya kushinda lakini kurudi hapa na kucheza vyema na kufanya vyema kila kitu ni jambo ambalo siwezi kulisahau," aliongeza gwiji huyo.