1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

The Daily Monitor lipo huru kuchapishwa Uganda

Admin.WagnerD30 Mei 2013

Siku kumi na moja baada ya kufungwa kwa gazeti la The Daily Monitor, nchini Uganda, hii leo asubuhi, waziri wa usalama wa nchi hiyo, Hillary Onek, alitangaza kuwa gazeti hilo sasa liko huru kuchapishwa tena

https://p.dw.com/p/18hJ8
Employees of the Daily Monitor newspaper with their mouths taped shut, take part in a protest against the closure of their premises by the Uganda government, outside their offices in the capital Kampala May 20, 2013. Police raided Uganda's leading independent newspaper on Monday and disabled its printing press after it published a letter about a purported plot to stifle allegations that Uganda President Yoweri Museveni is grooming his son for power, a senior editor said. The pen attached to the tape over the woman's mouth is a reference to the profession of journalism. REUTERS/James Akena (UGANDA - Tags: POLITICS MEDIA CIVIL UNREST)
Wafanyakazi wa Daily MonitorPicha: Reuters

Redio mbili zinazomilikiwa na gazeti hilo K-FM na Dembe FM nazo pia zimefunguliwa. Hata hivyo Gazeti jengine la Red Pepper ambalo pia lilifungwa bado halijafunguliwa lakini waziri Onek anasema mazunguumzo kati ya gazeti hio na serikali yanaendelea.

Akizungumza na waandishi habari mjini Kampala alisisitiza kuwa gazeti la The daily monitor lilivunja sheria ya usiri na kwa kufanya hivyo walikuwa wanahatarisha usalama wa nchi. Hio ndio sababu polisi ikaamua kutumia nguvu kuitafuta barua iliyoandikwa na mkuu wa vitengo vya ujasusi akidai kuwa kulikuwa na njama ya kuwauwa baadhi ya maafisa wakuu wa serikali na jeshi wanaopinga mpango wa Rais Yoweri Museveni wa kumwachia mamlaka mwanawe Brigedia Muhoozi Kaneirugaba.

Polisi wamendoka katika ofisi za gazeti

Baada ya siku kumi za vuta ni kuvute kati ya serikali na wakuu wa gazeti la The daily monitor, waziri Hillary Onek akatangaza kuwa polisi imewaondoa askari wake kwenye ofisi za The daily monitor ili waendelee na kazi zao kama kawaida wakati polisi ikiendelea na upelelezi wao na upekuzi.

Employees of the Daily Monitor newspaper with their mouths taped shut, sing slogans during a protest against the closure of their premises by the Uganda government, outside their offices in the capital Kampala May 20, 2013. Police raided Uganda's leading independent newspaper on Monday and disabled its printing press after it published a letter about a purported plot to stifle allegations that Uganda President Yoweri Museveni is grooming his son for power, a senior editor said. REUTERS/James Akena (UGANDA - Tags: POLITICS MEDIA CIVIL UNREST)
Wafanyakazi wa gazeti la Daily MonitorPicha: Reuters

Waziri Onek anasema wamelifungua gazeti hili baada ya wakuu wa gazeti hili kuomba msamaha kwa kuchapisha barua ambayo serikali inasema inahatarisha usalama wa nchi.

"Walituahidi kuwa gazeti la Monitor litachapisha ripoti ambazo wamezipata kwa njia inayofaa na za haki, pia watahakikisha ripoti zote watakazochapisha hazitaegemea upande wowote, hazitaibua hali ya wasi wasi nchini au kuchochea ukabila na chuki. Walituahidi kuwa hawatachapisha ripoti ambazo zitahatarisha usalama wa nchi na kutilia mkazo kuwa watakuwa wanazikagua kwa makini ripoti zinazohusu usalama wa nchi kabla ya kuchapishwa". alisema waziri Hillary Onek.

RedPepper bado kizuizini

Kuhusu kuendelea kufungwa gazeti la RedPepper, waziri Onek ameelza "Tumekuwa tukizungumza na RedPepper na leo tutakutana nao tena ili tuone ni vipi tunaweza kushirikiana. Ikiwa tutakubaliana nao kuwa watakuwa wanafanya kazi kulingana na sheria, hatutakuwa na shida kuwaruhusu waendelee kuchapisha".

Tukienda hewani, shirika la kutetea haki za waandishi habari nchini Uganda lilikuwa mahakamani kumshtaki mkuu wa polisi, mkuu wa sheria pamoja na taasisi ya mawasiliano kwa kukandamiza haki ya waandishi habari ya kuwa huru wanapofanya kazi yao. Sikiliza ripoti ya Leylah Ndinda kwa kubonyeza alama ya kusikiza masikioni hapo chini.

Mwandishi: Leylah Ndinda
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman