Thailand-maguruneti yafyetuliwa | Habari za Ulimwengu | DW | 30.11.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Thailand-maguruneti yafyetuliwa

Polisi yajaribu kuzungumza na wapinzani

Bankok:

Wapinzani zaidi ya 50 wa serikali ya Thailand wamejeruhiwa abaada ya gurumneti kuripuliwa.Shambulio hilo limezidisha makali ya mzozo unaoongozwa na wapinzani wa serikali nchini humo.Jengo la serikali linazingirwa na waafuasi wa upande wa upinzani tangu Agosti iliyopita.Wanadai waziri mkuu SOMCHAI WONGSAWAT ajiuzulu.Miripuko imeripotiwa pia katika kituo cha televisheni cha upande wa upinzani na karibu na uwanja wa ndege wa safari za ndani nchini.Watu wawili wamejeruhiwa.Viwanja vyote viwili vya ndege vinashikiliwa tangu siku kadhaa sasa na wapinzani.Jaribio la vikosi vya usalama kuwatimua wapinzani hao,limeshindwa.Duru za kuaminika kutoka Bankok zinazungumzia juhudi za polisi kuzungumza na wapinzani ili waondoke salama katika viwanja hivyo vya ndege.Wataalii laki mojua pamoja na wafanyabiashara wamekwama kufuatia kuzingirwa viwanja vya ndege nchini Thailand.

 • Tarehe 30.11.2008
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G6Cj
 • Tarehe 30.11.2008
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G6Cj
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com